Turibio wa Mongrovejo
Turibio wa Mongrovejo (16 Novemba 1538 – 23 Machi 1606) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Peru.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Inosenti XI tarehe 2 Julai 1679 halafu mtakatifu na Papa Benedikto XIII tarehe 10 Desemba 1726.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Turibio wa Mongrovejo alizaliwa nchini Hispania mnamo mwaka 1538.
Alijifunza sheria huko Salamanca, na mwaka 1580, akiwa bado mlei, aliteuliwa kuwa Askofu wa Lima nchini Peru, akaenda Amerika.
Alikuwa motomoto kwa kazi za kitume, akiitisha mikutano mbalimbali ili kurekebisha mambo ya dini na maadili na kukomesha makwazo ya waklero katika nchi nzima.
Kwa nguvu zote alitetea haki za Kanisa, mara kadhaa alitembelea, hasa kwa miguu, Wakristo wa jimbo lake pana, na kufanya kazi kwa muda mrefu kwa mafaa ya wenyeji wa Peru [2].
Alifariki dunia mwaka 1606.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 100-102
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 85-86
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "St. Toribio Alfonso Mogrovejo". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- TURIBIUS of Mogroveio Ilihifadhiwa 24 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- His biography at Lives of the Saints Ilihifadhiwa 10 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- (Kihispania) Short biography at MSN Encarta Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Archived 2016-05-18 at the Portuguese Web Archive
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |