Nenda kwa yaliyomo

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tamisemi)
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MamlakaTanzania
Makao MakuuDodoma
WaziriMohamed Omary Mchengerwa
Tovutitamisemi.go.tz

Ofisi wa Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (kifupi: TAMISEMI au OR-TAMISEMI) ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais na kusimamiwa na Waziri wa nchi akisaidiwa na manaibu wawili wao kama wasimamizi. Pia kuna Katibu mkuu ambaye yeye ni mtendaji Mkuu wa kila siku wa shughuli za serikali.[1]

Mojawapo ya kazi za Wizara hii ni kuratibu mipango yote ya maendeleo ya mikoa pamoja na Serikali za Mitaa chini ya uangalizi wa ofisi ya Rais.[2] Dhamana ya uendeshaji wa Wizara hii upo chini ya Waziri ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Tanzania.

Wizara hii imebeba dhamana ya maendeleo ya kimaeneo katika Mikoa na mitaa yake yote, hasa katika kuhakikisha kwamba miundombinu ya kila eneo kwenye ujenzi wa barabara na majumba inaendelea, tena kwa kiwango kilichostahili.[2]

Marejeo

  1. "Muundo wa Wizara".
  2. 2.0 2.1 "Majukumu ya Wizara".

Tazama pia

Viungo vya nje