Pande Mikoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Coordinates: 9°08′45″S 39°33′47″E / 9.14579°S 39.56299°E / -9.14579; 39.56299 Kwa kata kwenye Wilaya ya Muheza fungua hapa Pande

Pande Mikoma ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,596 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 65409.

Kata ya Pande Mikoma ina jumla ya vijiji 7 ambavyo ni Pande Plot, Nakimwera/Mikoma, Mtitimira, Namwedo, Songo Mnara, Malalani na Nang'oo Kiwala. Kata hiyo inapakana na kata ya Lihimalyao upande wa Kusini, kwa upande wa Kaskazini kuna bahari ya Hindi kuelekea Kilwa Masoko. Upande wa Magharibi kuna kata ya Mandawa na upande wa Mashariki kuna bahari ya Hindi.

Sehemu kubwa ya kata iko barani lakini kuna pia visiwa viwili vya Songo Mnara na Sanji ya Kati. Maghofu ya mji wa kihistoria ya Songo Mnara ni sehemu ya urithi wa dunia wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Wakazi wa kata hii ni wa makabila mchanganyiko: wapo Wamwera, Wamalindi, Wangoni, Wayao, Washirazi, Wamakonde na Wanyasa. Kata hii iko mwambao wa bahari ya Hindi, hivyo wakazi wake wana tamaduni za kimwambao. Ni wakarimu sana.

Wakazi wa eneo hilo shuguli zao kuu ni kilimo na uvuvi. Kwa upande wa kilimo wanalima mazao ya chakula ambayo ni muhogo, mtama, mahindi na mpunga na mazao ya biashara ambayo ni korosho na ufuta.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Lindi - Kilwa DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-04.
Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kijumbi | Kilwa Masoko | Kipatimu | Kivinje Singino | Kiranjeranje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Miteja | Mingumbi | Mitole | Namayuni | Miguruwe | Nanjirinji | Njinjo | Pande Mikoma | Somanga | Songosongo | Tingi (Kilwa)

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pande Mikoma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.

Songosongo ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,026 Msimbo wa posta ni 65420 [1] walioishi humo.