Songosongo

Majiranukta: 8°31′17″S 39°30′44″E / 8.52139°S 39.51222°E / -8.52139; 39.51222
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

8°31′17″S 39°30′44″E / 8.52139°S 39.51222°E / -8.52139; 39.51222


Pwani ya kisiwa cha Songosongo.

Songosongo ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Kata hii inafanywa na kijiji kimoja tu kilichopo kwenye kisiwa cha Songosongo kinachopatikana takriban kilomita 26 kutoka Kilwa Kivinje upande wa kaskazini mashariki kwenye Bahari Hindi.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,600 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,026 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 65420.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Songsongo ni nyumbani kwa jumuiya ya wavuvi. Kutokana na kukosa soko la samaki na uhaba wa vifaa vya kazi, wengi ni maskini; mnamo 2008 mapato ya wastani yalikuwa TSh 480,000 (wakati ule dollar 330 hivi) pekee kwa mwaka. [3]. Wenyeji wachache walipata ajira kwenye mradi wa gesi.

Mradi wa gesi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1974 gesi asilia iligunduliwa na kampuni ya AGIP kwenye kisiwa cha Songosongo na pia chini ya bahari karibu na kisiwa. Kwa miaka kadhaa ugunduzi haukufuatiliwa kwa sababu ya kukosa soko kwa matumizi yake.

Tangu mwaka 1995 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania pamoja na kampuni ya Globeleq (inayomilikiwa na taasisi za serikali za Uingereza na Norwei) zilianzisha kampuni mpya ya Songas. Songas ilijenga bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam kwa uzalishaji wa umeme[4]. Baada ya kukamilisha bomba, gesi ilianza kufika Dar mwaka 2004 inapotumiwa kwenye kituo cha umeme cha Ubungo.

Kwa mahitaji ya wilaya ya Kilwa ambayo haikuunganishwa bado na mtandao wa umeme wa kitaifa kituo kidogo cha umeme kilijengwa kwenye kata ya Somanga, Kilwa ambako umeme unatengenezwa kwa kutumia gesi kutoka bomba linalofika hapa barani kutoka kisiwa.

Baada ya kupatikana kwa gesi ya Songosongo maeneo ya ziada yalitambuliwa yenye gesi chini ya bahari.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Lindi - Kilwa DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-04. 
  3. Mashindano, Kibamba, Charle, Maro: Songosongo Social Services and Economic Survey (2008) www.tzonline.org/pdf/songosongsocialservices.pdf
  4. taarifa ya TPDC ya 16 Jul 2004
  5. Tanzania Natural Gas, tovuti ya Tanzaniinvest

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kinjumbi | Kipatimu | Kiranjeranje | Kivinje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Masoko | Miguruwe | Mingumbi | Miteja | Mitole | Namayuni | Nanjirinji | Njinjo | Pande | Somanga | Songosongo | Tingi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Songosongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.