Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MamlakaTanzania
Makao MakuuEneo la Chuo Kikuu cha Dodoma
WaziriGeorge Mkuchika
Tovutiutumishi.go.tz

Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais na kusimamiwa na Waziri chini ya utendaji wa Katibu Mkuu na Naibu Katibu mkuu ambao wote kwa pamoja wanaratibu shughuli za kila siku za Wizara hiyo.

Mojawapo ya majukumu ya wizara hiyo ni kusimamia misingi yote ya utumishi kwa kulinda maadili ya mtumishi wa umma.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazosimamia utawala bora, hivyo serikali ikaona umuhimu wa uwepo wa Wizara hiyo ambayo ipo chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais ni kama mwangalizi tu, kazi ikibaki chini ya waziri mwenye dhamana.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-06-17.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]