Nino wa Georgia
Nino wa Georgia (kwa Kigeorgia: წმინდა ნინო, ts'minda nino, kwa Kigiriki Αγία Νίνα, Agia Nina) alikuwa mwanamke (296 hivi – 338 au 340) aliyeingiza Ukristo nchini Georgia, na kwa sababu hiyo anaitwa "Aliye sawa na Mitume" na "Mwangazaji wa Georgia".
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake kwa kawaida huadhimishwa tarehe 14 Januari[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kadiri ya mapokeo alitokana na familia ya Kirumi yenye kuongea Kigiriki kutoka Kolastra, Kapadokia na alikuwa na undugu na Joji mfiadini,[2]. Kutoka Konstantinopoli alikwenda Iberia kwenye milima ya Kaukasi kama mfungwa.
Vyanzo vingine vinasema alitokea Roma, Yerusalemu au Galia (leo Ufaransa). [3]
Kwa utakatifu wa maisha yake alijivutia heshima ya wote na kisha kutenda miujiza ya uponyaji, alimfanya malkia Nana wa Iberia aongokee Ukristo.
Halafu mfalme Mirian III wa Iberia alirudishiwa uwezo wa kuona baada tu ya kumuomba "Mungu wa Nino", akaongoka pia na kufanya Ukristo kuwa dini rasmi ya nchi hiyo (327 hivi).
Nino aliendelea na umisionari nchini hadi kifo chake.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ "Orthodox Church of America -". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-20. Iliwekwa mnamo 2014-09-30.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-01. Iliwekwa mnamo 2014-09-30.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Wardrop, Margery (2006). Life of Saint Nino. Gorgias Press. ISBN 978-1-59333-471-0.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help) - Dowling, Theodore E. (2003). Sketches of Georgian Church History. Adamant Media. ISBN 978-1-4212-2891-4.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Biography from The St. Nina Quarterly Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Life of St Nino
- St. Nino church opening event in NYC Ilihifadhiwa 4 Desemba 2014 kwenye Wayback Machine.
- The Church of St. Nina, Kandalaksha, Murmansk oblast, Russia. English summary Ilihifadhiwa 21 Mei 2018 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |