Mzee Majuto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Amri Athumani
King Majuto portrait.jpg
Amezaliwa Amri Athuman
1 Agosti 1948 (1948-08-01) (umri 73)
Tanga, Tanzania
Amekufa Agosti 8, 2018 (umri 70) Dar es Salaam, Tanzania
Jina lingine King Majuto
Kazi yake Muigizaji, Mtunzi, Mchekeshaji, Muongozaji Mwandishi

Alhaji Amri Athumani (alijulikana sana kwa jina la King Majuto na pia Mzee Majuto[1]; Tanga, (1 Agosti 1948 - Dar es Salaam, 8 Agosti 2018) alikuwa mwigizaji, mwongozaji, mwandishi wa muswada na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania.

Ndiye mwigizaji wa kwanza kurekodi mikanda yake na kuiuza huku akifanya kazi na Shirika la Filamu Tanzania (Tanzania Film Company-TFC)[2][3].

Wasifu wake[hariri | hariri chanzo]

Alisoma shule ya Msambwini iliyoko mkoani Tanga.

Alianza kuigiza mnamo mwaka 1958 (akiwa na umri wa miaka 9 mpaka 10); wakati huo alikuwa akiigiza katika majukwaa. [4]

Matibabu yake nchini India[hariri | hariri chanzo]

Aprili 28, 2018 Waziri wa habari, sanaa na michezo, Harrison Mwakyembe alimtembelea Mzee Majuto katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika siku hiyo Waziri Mwakyembe alitangaza nia ya serikali ya Tanzania kumpeleka Mzee Majuto nchini India. Awali King Majuto aliripotiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume ambapo alianza matibabu yake nchini Tanzania [5]

Mnamo Mei 1, Mzee Majuto aliripotiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi[6] .[7][8][9]

Kuzidiwa na kifo chake[hariri | hariri chanzo]

Alitibiwa India hadi hapo afya yake ilipoimarika na kurejea nchini Tanzania kuendelea na kliniki yake katika hospitali ya Muhimbili.

Baadaye Mzee Majuto aliripotiwa kuzidiwa, hali iliyopelekea kulazwa tena hospitali ya taifa Muhimbili katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU)

Alipatwa na mauti hapo 8 Agosti 2018 majira ya saa mbili kamili usiku katika wodi za mwaisera, katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]

Zifuatazo ni filamu anazodaiwa kushiriki kuigiza enzi za uhai wake.

 • Lolita
 • Sio Sawa
 • Mama Ntilie
 • Nahama
 • Gumzo
 • Mrithi Wangu
 • Rent House
 • Ndoa ya Utata
 • Daladala
 • Nimekuchoka
 • Mbegu
 • Zebra
 • Shikamoo Mzee
 • Tabia
 • Utani
 • Tikisa
 • Trouble Maker
 • Gundu
 • Kizungunguzu
 • Shoe Shine
 • Street Girl
 • Faithful
 • Mtego wa Panya
 • Boss
 • Back with Tears
 • Sikukuu ya Wajinga
 • Nyumba Nne
 • Chips Kuku
 • Kitu Bomba
 • Ndoto ya Tamaa
 • Lakuchumpa
 • ATM
 • Bishoo
 • Tupo Wangapi
 • Moto Bati
 • Varangati
 • Out Side
 • Pusi na Paku
 • Juu kwa Juu
 • Swagger
 • Oh Mama
 • Jazba
 • Mke wa Mtu Sumu
 • Mbugila
 • Kidumu
 • Mkali Mo
 • Mpela Mpela
 • Utanibeba
 • Babatan
 • Mjomba
 • Msela wa Manzese
 • Karaha
 • Mpango Sio Matumizi
 • Mume Bwege
 • Shuga Mammy,
 • Embe Dodo
 • Nakwenda Kwa Mwanangu
 • Seaman
 • Naja Leo Naondoka Leo Tanga
 • Mgeni Njoo
 • Kuwadi
 • Kulipa Tabu
 • Uso wa Mbuzi
 • Machimbo
 • Fundi Feni
 • Mwizi wa Kuku
 • Mtu Mzima Hovyo
 • Wake Up
 • Vituko Show Vol. 10
 • Bettery Low
 • Brothers
 • Alosto
 • Back from New York
 • Kipofu
 • Koziman Vol 21
 • After Money
 • Talaka Yangu
 • Gereji
 • Welcome Back
 • Mshamba
 • Pedeshee
 • Waiter
 • Inye Plus
 • Inye Gwedegwede
 • Inye Vol.1

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzee Majuto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.