Aljeri : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Removing Link FA template (handled by wikidata)
No edit summary
Mstari 17: Mstari 17:
}}
}}


[[Picha:Sm Bombardment of Algiers, August 1816-Luny.jpg|thumb|right|260px|Waingereza walivamia meli za maharamia Algiers mwezi wa Agosti 1816]]
[[Picha:Sm Bombardment of Algiers, August 1816-Luny.jpg|thumb|right|260px|Waingereza walivamia meli za maharamia Algiers mnamo Agosti 1816.]]
[[Picha:Algeri04.jpg|thumb|260px|Majengo ya nyakati za ukoloni]]
[[Picha:Algeri04.jpg|thumb|260px|Majengo ya nyakati za ukoloni.]]
[[Picha:Algeri08.jpg|thumb|right|260px|Mtaa wa Algiers mwambaoni]]
[[Picha:Algeri08.jpg|thumb|right|260px|Mtaa wa Algiers mwambaoni.]]
[[Picha:Algeri06.jpg|right|thumb|260px|Uwanja wa "Mashahidi wa Uhuru"]]
[[Picha:Algeri06.jpg|right|thumb|260px|Uwanja wa "Mashahidi wa Uhuru".]]
[[Picha:Algiersnasa.jpg|right|260px|Algiers inavyonekana kutoka angani]]
[[Picha:Algiersnasa.jpg|right|260px|Algiers inavyoonekana kutoka angani.]]


'''Algiers''' ([[Kiarabu]] '''مدينة الجزائر''', ''madīnat al-djazā'ir'' ("mji wa visiwa"), [[Kifaransa]] ''Alger'') ni [[mji mkuu]] pia mji mkubwa kabisa wa nchi [[Algeria]] ikiwa na wakazi milioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni tano. Iko mwambaoni wa [[Mediteranea]].
'''Algiers''' (kwa [[Kiarabu]] '''مدينة الجزائر''', ''madīnat al-djazā'ir'', "mji wa visiwa"; kwa [[Kifaransa]] ''Alger'') ni [[mji mkuu]] pia mji mkubwa kabisa wa nchi ya [[Algeria]] ikiwa na wakazi [[milioni]] 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni 5. Iko [[Mwambao|mwambaoni]] mwa [[bahari]] ya [[Mediteranea]].

Algiers ni makao ya serikali na kitovu cha uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano nchini.
Algiers ni makao ya [[serikali]] na [[kitovu]] cha [[uchumi]], [[biashara]], [[utamaduni]] na [[mawasiliano]] nchini.


== Historia ==
== Historia ==
Mji ulianzishwa kama koloni ya [[Wafinisia]] katika karne ya 4 [[KK]]. Mahali palifaa kutokana na visiwa vinne vidogo vilivyokuwepo karibu na mwambao (lakini katika karne ya 17 [[BK]] viliunganishwa na bara). Baada ya kuenea kwa [[Dola la Roma]] ikawa mji wa Icosium na kuvamiwa na [[Waarabu]] [[Waislamu]] mwaka 702. Waberber wa kabila la Beni Mezghenna walikaa katika eneo hili. Mwaka 960 kiongozi wa Kiberber [[Buluggin ibn Ziri]] aliyekuwa gavana ya makhalifa wa Fatimiya wa Misri aliteua mahali pa Icosium na kujenga boma hapa. Mji uliitwa sasa "Al-djazair-Mezghenna" yaani "visiwa vya Beni Mezghenna". Hapa ndipo asili ya jina la leo "Al djaza'ir (الجزائر)" yaani "visiwa".
Mji ulianzishwa kama [[koloni]] la [[Wafinisia]] katika [[karne ya 4 KK]]. Mahali palifaa kutokana na visiwa vinne vidogo vilivyokuwepo karibu na mwambao (lakini katika [[karne ya 17]] [[BK]] viliunganishwa na bara).
Katika karne zilizofuata mji ulivamiwa na watawala [[Wamurabitun]] na [[Wamuwahidun]] kutoka [[Moroko]]. Baadaye mji ukawa chini ya masultani wa Algeria ya Kaskazini.


Baada ya kuenea kwa [[Dola la Roma]] ikawa mji wa Icosium na kuvamiwa na [[Waarabu]] [[Waislamu]] mwaka [[702]]. [[Waberber]] wa [[kabila]] la Beni Mezghenna walikaa katika eneo hili. Mwaka [[960]] kiongozi wa Kiberber [[Buluggin ibn Ziri]] aliyekuwa [[gavana]] wa [[makhalifa]] wa [[Fatimiya]] wa [[Misri]] aliteua mahali pa Icosium na kujenga [[boma]] hapa. Mji uliitwa sasa "Al-djazair-Mezghenna" yaani "visiwa vya Beni Mezghenna". Ndiyo [[asili]] ya [[jina]] la leo "Al djaza'ir (الجزائر)" yaani "visiwa".
Mnamo mwaka 1302 [[Hispania]] ilifaulu kushika visiwa vidogo mwambanoni kwa miaka kadhaa hadi kufukuzwa tena na mharamia [[Barbarossa]] aliyeteka mji kwa niaba ya Sultani wa [[Uturuki]]. Tangu karne ya 16 BK Algiers ikawa mji wa kujitawala ndani ya [[Dola la Uturuki]]. Imekuwa mara kwa mara makao makuu ya [[uharamia|maharamia]] ya Mediteranea ya magharibi. Maharamia hawa walishambulia jahazi za Wakristo kama [[Waitalia]], [[Wafaransa]], [[Wahispania]] na kadhalika na kuteka abiria pamoja na mabaharia. Waliuzwa kama [[watumwa]] au kurudishwa kwao baada ya kulipa pesa. Maharamia waliweza pia kushambulia miji ya Wakristo mwambaoni wa Mediteranea na kutwaa wakazi kama watumwa. Hali hiyo ilisababisha tena na tena majaribio ya nchi za [[Ulaya]] kuvamia Algiers lakini bila kufaulu hadi karne ya 19. Mwaka 1815 [[Marekani]] ilishambulia Algiers baada ya kupotea meli na raia kwa maharamia wa mji; mwaka 1816 [[Waingereza]] pamoja na [[Waholanzi]] walishambilia tena kwa kusudi ya kulinda meli na raia zao. Walifaulu kumlazimisha mtawala wa Algiers atie sahihi kwenye mkataba wa kutochukua tena Watumwa kutoka nchi za Ulaya ingawa biashara hii iliendelea kwa siri hata baadaye.


Katika [[karne]] zilizofuata mji ulivamiwa na [[watawala]] [[Wamurabitun]] na [[Wamuwahidun]] kutoka [[Moroko]]. Baadaye ukawa chini ya [[Sultani|masultani]] wa Algeria ya Kaskazini.
Mwaka 1830 Wafaransa walivamia mji na kuanzisha utawala uliokuwa mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa katika Algeria.


Mnamo mwaka [[1302]] [[Hispania]] ilifaulu kushika visiwa vidogo mwambaoni kwa miaka kadhaa hadi kufukuzwa tena na mharamia [[Barbarossa]] aliyeteka mji kwa niaba ya Sultani wa [[Uturuki]].
Wafaransa walipanusha na kubadilisha mji wa Kiarabu na Kiberber. Katika karne ya 19 Wafaransa wengi walihamia Algeria hadi Algiers ilikuwa mji mwenya wakazi wengi Wafaransa kuliko wenyeji asilia waliokaa hasa katik mji wa kale ulioitwa "Kasbah". Wafaransa waliozaliwa Algeria walijiita "pieds noir" (miguu meusi).
Wakati wa [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]] Alegria ilikuwa chini ya serikali ya Kifaransa katika maeneo yasiyovamiwa na Ujerumani hadi kuingiliwa na wanajeshi Waamerika na Waingereza mwaka 1942. Baadaye ikawa mji mkuu wa "Ufaransa Huru" hadi mwisho wa vita.


Tangu [[karne ya 16]] BK Algiers ikawa mji wa kujitawala ndani ya [[Dola la Uturuki]]. Imekuwa mara kwa mara [[makao makuu]] ya [[uharamia|maharamia]] wa Mediteranea ya magharibi. Maharamia hao walishambulia [[jahazi]] za [[Wakristo]] kama [[Waitalia]], [[Wafaransa]], [[Wahispania]] na kadhalika na kuteka [[abiria]] pamoja na [[Baharia|mabaharia]]. Waliuzwa kama [[watumwa]] au kurudishwa kwao baada ya kulipiwa [[pesa]]. Maharamia waliweza pia kushambulia miji ya Wakristo mwambaoni mwa Mediteranea na kutwaa wakazi kama watumwa. Hali hiyo ilisababisha tena na tena majaribio ya nchi za [[Ulaya]] kuvamia Algiers lakini bila kufaulu hadi [[karne ya 19]].
Tangu uhuru wa Algeria 1962 Algiers imekuwa mji mkuu wa Algeria. Akina pieds noir walio wengi waliondoka wakihofia uchungu baada ya vita ya ukombozi.

Mwaka [[1815]] [[Marekani]] ilishambulia Algiers baada ya kupotea [[meli]] na [[raia]] kwa maharamia wa mji; mwaka [[1816]] [[Waingereza]] pamoja na [[Waholanzi]] walishambulia tena kwa kusudi la kulinda meli na raia zao. Walifaulu kumlazimisha mtawala wa Algiers atie [[sahihi]] [[mkataba]] wa kutochukua tena watumwa kutoka nchi za Ulaya ingawa [[biashara]] hii iliendelea kwa siri hata baadaye.

Mwaka [[1830]] Wafaransa walivamia mji na kuanzisha utawala uliokuwa mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa katika Algeria.

Wafaransa walipanua na kubadilisha mji wa Kiarabu na Kiberber. Katika karne ya 19 Wafaransa wengi walihamia Algeria hadi Algiers ilikuwa mji mwenye wakazi wengi Wafaransa kuliko wenyeji waliokaa hasa katika mji wa kale ulioitwa "Kasbah". Wafaransa waliozaliwa Algeria walijiita "pieds noir" (miguu myeusi).

Wakati wa [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]] Algeria ilikuwa chini ya [[serikali]] ya Kifaransa katika maeneo yasiyovamiwa na [[Ujerumani]] hadi kuingiliwa na [[wanajeshi]] Wamarekani na Waingereza mwaka [[1942]]. Baadaye ikawa mji mkuu wa "[[Ufaransa Huru]]" hadi mwisho wa [[vita]].

Tangu [[uhuru]] wa Algeria ([[1962]]) Algiers imekuwa mji mkuu wa Algeria. Akina pieds noir walio wengi waliondoka wakihofia uchungu baada ya [[vita vya ukombozi]].


== Marejeo ==
== Marejeo ==
{{marejeo}}
{{marejeo}}


==Viungo vya nje==
{{mbegu-jio-Algeria}}
{{Commons}}
{{Commons}}
{{mbegu-jio-Algeria}}


[[Jamii:Algeria]]
[[Jamii:Algeria]]
[[Jamii:Miji ya Algeria]]
[[Jamii:Miji ya Algeria]]
[[Jamii:Miji Mikuu Afrika]]
[[Jamii:Miji Mikuu Afrika]]
[[Jamii:Miji ya pwani la Mediteranea]]
[[Jamii:Miji ya pwani ya Mediteranea]]
[[Jamii:Algiers| ]]
[[Jamii:Algiers| ]]
[[Jamii:Miji ya Dola la Roma]]
[[Jamii:Miji ya Dola la Roma]]

Pitio la 10:36, 8 Desemba 2018








Jiji la Algiers

Nembo
Nchi Algeria
Jimbo Jimbo ya Algiers
Waingereza walivamia meli za maharamia Algiers mnamo Agosti 1816.
Majengo ya nyakati za ukoloni.
Mtaa wa Algiers mwambaoni.
Uwanja wa "Mashahidi wa Uhuru".
Algiers inavyoonekana kutoka angani.
Algiers inavyoonekana kutoka angani.

Algiers (kwa Kiarabu مدينة الجزائر, madīnat al-djazā'ir, "mji wa visiwa"; kwa Kifaransa Alger) ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa wa nchi ya Algeria ikiwa na wakazi milioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni 5. Iko mwambaoni mwa bahari ya Mediteranea.

Algiers ni makao ya serikali na kitovu cha uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano nchini.

Historia

Mji ulianzishwa kama koloni la Wafinisia katika karne ya 4 KK. Mahali palifaa kutokana na visiwa vinne vidogo vilivyokuwepo karibu na mwambao (lakini katika karne ya 17 BK viliunganishwa na bara).

Baada ya kuenea kwa Dola la Roma ikawa mji wa Icosium na kuvamiwa na Waarabu Waislamu mwaka 702. Waberber wa kabila la Beni Mezghenna walikaa katika eneo hili. Mwaka 960 kiongozi wa Kiberber Buluggin ibn Ziri aliyekuwa gavana wa makhalifa wa Fatimiya wa Misri aliteua mahali pa Icosium na kujenga boma hapa. Mji uliitwa sasa "Al-djazair-Mezghenna" yaani "visiwa vya Beni Mezghenna". Ndiyo asili ya jina la leo "Al djaza'ir (الجزائر)" yaani "visiwa".

Katika karne zilizofuata mji ulivamiwa na watawala Wamurabitun na Wamuwahidun kutoka Moroko. Baadaye ukawa chini ya masultani wa Algeria ya Kaskazini.

Mnamo mwaka 1302 Hispania ilifaulu kushika visiwa vidogo mwambaoni kwa miaka kadhaa hadi kufukuzwa tena na mharamia Barbarossa aliyeteka mji kwa niaba ya Sultani wa Uturuki.

Tangu karne ya 16 BK Algiers ikawa mji wa kujitawala ndani ya Dola la Uturuki. Imekuwa mara kwa mara makao makuu ya maharamia wa Mediteranea ya magharibi. Maharamia hao walishambulia jahazi za Wakristo kama Waitalia, Wafaransa, Wahispania na kadhalika na kuteka abiria pamoja na mabaharia. Waliuzwa kama watumwa au kurudishwa kwao baada ya kulipiwa pesa. Maharamia waliweza pia kushambulia miji ya Wakristo mwambaoni mwa Mediteranea na kutwaa wakazi kama watumwa. Hali hiyo ilisababisha tena na tena majaribio ya nchi za Ulaya kuvamia Algiers lakini bila kufaulu hadi karne ya 19.

Mwaka 1815 Marekani ilishambulia Algiers baada ya kupotea meli na raia kwa maharamia wa mji; mwaka 1816 Waingereza pamoja na Waholanzi walishambulia tena kwa kusudi la kulinda meli na raia zao. Walifaulu kumlazimisha mtawala wa Algiers atie sahihi mkataba wa kutochukua tena watumwa kutoka nchi za Ulaya ingawa biashara hii iliendelea kwa siri hata baadaye.

Mwaka 1830 Wafaransa walivamia mji na kuanzisha utawala uliokuwa mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa katika Algeria.

Wafaransa walipanua na kubadilisha mji wa Kiarabu na Kiberber. Katika karne ya 19 Wafaransa wengi walihamia Algeria hadi Algiers ilikuwa mji mwenye wakazi wengi Wafaransa kuliko wenyeji waliokaa hasa katika mji wa kale ulioitwa "Kasbah". Wafaransa waliozaliwa Algeria walijiita "pieds noir" (miguu myeusi).

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Algeria ilikuwa chini ya serikali ya Kifaransa katika maeneo yasiyovamiwa na Ujerumani hadi kuingiliwa na wanajeshi Wamarekani na Waingereza mwaka 1942. Baadaye ikawa mji mkuu wa "Ufaransa Huru" hadi mwisho wa vita.

Tangu uhuru wa Algeria (1962) Algiers imekuwa mji mkuu wa Algeria. Akina pieds noir walio wengi waliondoka wakihofia uchungu baada ya vita vya ukombozi.

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aljeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.