Dameski : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
No edit summary |
||
Mstari 49: | Mstari 49: | ||
Mji wa kisasa una eneo la 105 km2. Eneo la 77 km2 limetumiwa kwa majengo, makazi na mashamba, na eneo lililobaki ni mlima wa Qassioun. |
Mji wa kisasa una eneo la 105 km2. Eneo la 77 km2 limetumiwa kwa majengo, makazi na mashamba, na eneo lililobaki ni mlima wa Qassioun. |
||
=== |
=== Hali ya Hewa === |
||
Kwa sababu ya milima ya Anti-Lebanon, kuna mvua chache mjini. Wakati wa baradi, kuna mvuva na theluji mara kwa mara. Wakati wa joto, hali ya hewa ni kavu na joto. |
Kwa sababu ya milima ya Anti-Lebanon, kuna mvua chache mjini. Wakati wa baradi, kuna mvuva na theluji mara kwa mara. Wakati wa joto, hali ya hewa ni kavu na joto. |
||
Pitio la 19:15, 22 Juni 2017
Mkoa | Dameski |
Anwani ya kijiografia | 33°30'35" N; 36°18'33"E |
Kimo | 690 m juu ya UB |
Eneo | 105 km² |
Wakazi | 1.580.909 (2006) |
Msongamano wa watu | watu 15.056/km² |
Simu | 963 (nchi), 11 (mji) |
Lage | |
Dameski (pia: Damasko, Damaskus, Damascus; kiar.: دمشق "dimashk") ni mji mkuu wa Syria, pia ni mji mkubwa wa nchi hiyo wenye wakazi milioni 4.5.
Dameski ni kati ya miji ya kale kabisa duniani iliyoendelea kukaliwa mahali palepale: inaaminiwa imekaliwa tangu miaka 8,000 au zaidi.
Jina
Nchini mji huitwa mara nyingi الشام ("ash-shām"). Jina hilo latumiwa na Waarabu wengine pia kwa nchi yote ya Syria. Kihistoria "Shamu" ilikuwa jina la nchi yote upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.
Haijulikani kutoka lugha gani jina la “Dameski” lilikujaa. Dameski inaitwa na waenyeji wake kwa jina la “Sham” pia au wakati nyingine “al Fayhaa” au "madinat al yasamin," kwa Kiarabu, yaani “Mji wa Yasimini.”
Jiografia
Dameski iko takriban kilometa 80 mashariki ya pwani ya Mediteranea na kilometa 30 kutoka mpaka kati ya Syria na Lebanoni kando ya mto Barada. Iko kwenye kimo cha mita 680 juu ya UB.
Upande wa magharibi ni milima ya Libanoni ndogo inayozuia mawingu yenye mvua kufika kutoka Mediteranea. Upande wa mashariki inaanza jangwa. Kati ya mji, kuna mito midogo mingi, na mto mkuu ni mto wa Barada.
Zamani, palikuwa na bustani nyingi sehemu zote za nchi. Lakini kwa sababu ya uchafuzi wa mazingira na idadi ya watu ambayo imekuwa inapanda , siku hizi bustani ni chache na pia hakuna maji mengi mitoni kwa mji.
Mji wa kisasa una eneo la 105 km2. Eneo la 77 km2 limetumiwa kwa majengo, makazi na mashamba, na eneo lililobaki ni mlima wa Qassioun.
Hali ya Hewa
Kwa sababu ya milima ya Anti-Lebanon, kuna mvua chache mjini. Wakati wa baradi, kuna mvuva na theluji mara kwa mara. Wakati wa joto, hali ya hewa ni kavu na joto.
Historia
Akiolojia imeonyesha makazi ya kibinadamu katika eneo la Dameski tangu milenia ya 5 KK.
Utawala wa Misri
Mji ulitajwa mara ya kwanza kimaandishi kwa jina la "Tamasqu" (tmsq) katika taarifa za Misri ya Kale wakati wa Farao Thutmosis III (1479 KK - 1425 KK). Ilikuwa chini ya utawala wa Misri hadi mnamo mwaka 1100 KK.
Ufalme wa Aramu
Tangu 1000 KK mji ukawa kitovu cha ufalme wa Aramu-Dameski unaotajwa pia mara nyingi katika Biblia. Baada ya kushindana mara nyingi na Israeli ulikwisha katika vita dhidi ya Assyria mwaka 732 KK.
Utawala wa Babeli, Uajemi, Wagiriki na Roma
Assyria ilishindwa na Nebukadreza II wa Babeli na Dameski ikawa sehemu ya milki ya pili ya Babeli tangu 572 KK.
Mwaka 538 KK Uajemi iliPOchukua nafasi ya Babeli Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Syria.
Kufika kwa Aleksanda Mkuu tangu 333 KK kulibadilisha siasa ya Mashariki ya Kati na Dameski ikawa sehemu ya dunia ya Kigiriki.
Wafuasi wa Aleksander waliendelea kushindania mji baadaye: mara ukawa upande wa Waptolemayo (Misri) mara upande wa Waseleukido.
Tangu 64 KK Dola la Roma likaingia Shamu. Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Kiroma likakua na kustawi. Mpangilio wa Waroma yameonekana hadi leo katika mji wa Kale wa Dameski hata kama majengo ya nyakati zile yamefichwa mita 5 chini ya uwiano wa mji wa leo. Barabara ya decumanus ya Kiroma, ambayo imetajwa katika Biblia kama "barabara iliyonyoka" au "barabara iitwayo Nyofu" (Mdo 9,11), inaoonekana hadi leo.
Kaisari Theodosio I alijenga kanisa kubwa la Mt. Yohane lililotunza kichwa cha Yohane Mbatizaji.
.
Waarabu na Waosmani
Dameski ilivamiwa na jeshi la Waarabu Waislamu chini ya khalifa Umar I mwaka 636 B.K.. Kanisa la Mt. Yohane likabadilihswa kuwa msikiti mkuu. Baada ya ushindi wa Muawiyya mwaka 661 juu ya Hussain ibn Ali alichukua cheo cha khalifa akikaa Dameski. Hivyo mji ukawa mji mkuu wa milki ya Wamuawiya iliyotawala nchi kati ya Hispania hadi milango ya China.
Khalifa wa mwisho wa Wamuawiya Marwan II alihamisha makao yake kwenda Haran katika Mesopotamia ya kaskazini. Marwan alishindwa baadaye na Abu al-`Abbās `Abdu'llāh as-Saffāh aliyeanzisha utawala wa makhalifa Waabbasi na kupeleka mji mkuu Baghdad. Dameski haikurudishwa tena umuhimu na heshima jinsi ilivyokuwa wakati wa Wamuawiya.
Iliendelea kuwa maKao makuu ya kijimbo tu, isipokuwa kwa vipindi vifupi ilipokuwa mji huru tena pasipokuwa na utawala wenye nguvu ya makhalifa.
Salah-ad-Din aliweka mji tena chini ya utawala wa Misri hadi 1516. Mnamo 1400 Dameski ilivamiwa na kuharibiwa kabisa na Timur.
Utawala wa Milki ya Waturuki Waosmani ulianza 1516 ukaendelea hadi 1918. Dameski ilijikuta tena mbali na mji mkuu wa milki huko Istanbul. Ilikuwa na umuhimu fulani kwa sababu misafara ya hija kwenda Maka ilianzia Dameski.
Mwaka 1516, kiongozi Mmisrowa Dameski alikimbia mji. Baada siku chache, Sultan Selim I alifika mjini akaweka mji juu ya Waosmani. Wakati ambapo Selim I alirudi Dameski, alijenga msikiti mpya, tekkiye (ni kama soko), na kaburi ya Shaikh Muhi al Din ibn Arabi mtaani kwa Al Salhiyeh.
Waosmani walitawala Dameski kwa muda ya miaka 400. Lakini baina mwaka 1832 na mwaka 1840 ilitawaliwa na Wamisri. Licha ya udogo wake na kwa sababu ya mahali kwake katika njia ya Hajj, Dameski ilikuwa mji muhimu kwa serikali ya Kiosmani. Mwaka 1560, Waosmani walijenga Tikkeyeh Suleymaniyeh ambapo wasafiri na wafanya Hajj waliweza kustarehe.
Wakati wa utawala wa Waosmani, Wayahudi na Wakristo wa Dameski walikuwa dhimmi (watu siyo Waislamu na walilazimisha kulipa kodi tofauti kuliko Waislamu) na waliweza kuendelea na dini zao.
Mwanzo wa karne ya 20, uwazo wa utaifa wa Kiarabu ulianza Dameski kwa sababu ya sheria kutoka Istanbul ambazo zilitumiwa zibadilishe Dameski “mji mturuki” zaidi. Utekelezaji wa watu wenye elimu mwaka 1915 na mwaka 1916 uliongeza uwazo huu wa utaifa wa Kiarabu. Mwaka 1918, Mapinduzi ya Waarabu alianza nchini kwa Syria na baada ya wakati chache, Waosmani waliondoka Syria na Waingereza walichukua nchi. Faisal ibn Hussein alikuwa mfalme mpya wa Syria. Mwaka 1920, serikali iliandika katiba mpya ya kidemokrasia. Lakini, mwaka 1920, Mkutano wa Versailles aliutoa Ufaransa nchi ya Syria kama ukoloni wake. Ufaransa uliingia Syria mwaka 1920.
Mwaka 1925, mapinduzi mapya ambayo ulianzishwa na Hauran (eneo la mashamba kusini ya nchi) yalifika Dameski. Wasyria walitaka uhuru wao. Lakini, Ufaransa ulitupa mabombu Dameski na waliacha mapinduzi. Wakati wa Vita Kuu ya Dunya II, Syria jeshi la Ufaransa Uhuru na jeshi la Uingereza, walichukua Dameski. Baada ya Vita, Ufaransa ulitoa Syria uhuru na Dameski ilikuwa mji mkuu wa nchi mpya.
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivunja milki ya Waosmani ikaleta utawala wa Ufaransa katika Syria.
Mji Mkuu wa Syria huru
Uhuru wa Syria mwaka 1946 ulifanya Dameski mji mkuu wa nchi huru. Tangu hapo Dameski ikakua sana ikawa mji wa viwanda na biashara.
Uchumi
Zamani, Dameski ulikuwa mji muhimu wa biashara. Mpaka sasa, biashara ni muhimu mjini. Kuna masoko na kampuni nyingi. Kwa sababu ya vita vya Syria, Dameski ni mji mkuu wa uchumi wa Syria.
Kuna viwanda vya serikali mjini. Lakini viwanda vya binafsi ni vichache. Kwa sababu ya vita, kuna sasa viwanda vichache kuliko zamani. Lakini kwa sababu ya kuntengwa kwa nchi kutokana na sababu mbalimbali na pia kwa sababu ya vita vya uraia, hakuna uchumi wenye nguvu. Kuna ufakiri wingi na ukosefu wa ajira.
Taarifa za Wakazi
Mwaka wa 2011, idadi ya watu ilikuwa 1,711,000. Lakini, kuna miji midogo karibu sana na Dameski kama Duma, Harasta, Daraya, Jaramana, na Tal. Kwa jumla kuna watu zaidi 5 milioni wanaoishi kanda ya Dameski. Hasa, baada ya vita vya uraia, kuna watu wengi kuliko kila mahali kwa Syria waliohamia Dameski.
Dameski kuna mchanganyiko wa watu. Karibu watu wote ni Waarabu na Waislamu, hasa Wasunni. Lakini, kuna watu wakristo, waalawi, waarmenia, na kadhalika. Lugha nyingi zinazosemwa mjini ni kiarmenia, kiarabu, kifaransa, na kiaramaic. Zamani, palikuwa na wayahudi wengi mjini lakini waliondoka baada ya kuanzishwa kwa nchi ya Israel.
Mji wa Kale na Utamaduni
Mji wa Dameski wa Kale ni mji wa kipekeeduniani. Mji unajulikana kwa barabara ndogo zake, zinapopatikana masoko, makasri, misikiti, makanisa yake. Mji wa kale ni mchanganyiko wa magofu ya Warumi, Waosmani, and Wafaransa. Maisha ndani ya mji wa Dameski yafanana na maisha ya watu wa zamani.
Milango saba ya mji:
Bab al-Faradis
Mlango al-Salam
Bab Tuma
Bab Sharqi
Bab Kisan
Bab al-Saghir
Bab al-Jabiyeh
Makanisa maalum:
Kanisa la Mtakatifu Paul
Nyumba ya Mtakatifu Ananias
Kanisa la Kimarimia
Kanisa Katoliki la Kirumi
Kanisa la Mtakatifu John
Kanisa Ortodoks la Mtakatifu George
Misikiti Maalum
Msitiki wa Waomaya (Mahali ambapo ni kaburi ya Salaheddin, shujaa mwislamu maalum sana)
Msitiki wa Sayyida Ruqaya
Msikiti wa Sinaniya
Msikiti wa Toba
Khan (mahali ambapo wasafiri waliweza kustarehe)
Khan Jaqmaq
Khan Asaad Pasha
Khan Suleyman Pasha
Nyuma muhimu na Makasri
Kasri la Azem
Beit al-Aqqad
Maktab Anbar
Beit al-Mamlouka
Elimu
Dameski ni pahali pa elimu Syria. Chuo Kikuu cha Dameski ni chuo kikuu kikubwa na ya zamani zaidi nchini. Baada ya sheria, ambaye iliruhusu vyuo vikuu vya binafsi, kuna vyuo vikuu vipya kama: Syrian Virtual University, Chuo Kikuu cha Qalamoun, n.k.
Usafirishaji
Uwanja wa ndege mkuu ni Uwanja wa Ndege wa Dameski uko karibu na mji. Lakini, kwa sababu ya vita vya uraia, kuna ndege chache tu ambazo zinasafiri Dameski.
Hakuna huduma za usafirishaji kubwa. Kuna njia za basi ndogo. Wakazi wa mji wanategemea “microbus.” Microbus ni kama matatu ya Kenya au dala dala za Tanzania. Dameski, kuna njia zaidi ya mia moja ya microbus mjini. Microbus zinaenda kila mahali kwa mji.
Kuna pia shirika la “Chemin de Fer Syriens” ambalo ni shirika la treni. Lakini baada ya vita vya uraia, hakuna treni zo zote nchini.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Dameski kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |