Nenda kwa yaliyomo

Theodosius Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Theodosio I)
Sarafu yenye sura ya Kaizari Theodosius I.

Flavius Theodosius (11 Januari, 34717 Januari, 395) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 15 Mei, 392 hadi kifo chake.

Kabla hajatawala dola zima, alikuwa Kaizari upande wa Mashariki kuanzia Agosti 378. Upande wa Mashariki alimfuata Valens.

Theodosius alikuwa Kaizari wa mwisho aliyetawala dola zima la Roma. Ndiye aliyetangaza Ukristo wa Kikatoliki kuwa dini rasmi ya dola.

Hati ya Thesalonike ilisisitiza imani moja tu kuwa halali katika dola la Roma, ile "katholiki" (yaani, isiyo ya sehemu) na "orthodoksi" (yaani, sahihi).

Tangu hapo, Theodosius alitumia nguvu nyingi kuzima aina zote za Ukristo tofauti na hiyo, hasa Uario.[1]

Hati hiyo ilifuatwa mwaka 381 na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli, uliothibitisha na kuongezea ungamo la Nisea katika Kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli.[2]

Mwaka 383, Kaisari alidai madhehebu mengine yote yampatie maungamo yao ya imani, akayachambua na kuyachoma yote isipokuwa ya Wanovasyani. Hivyo madhehebu hayo hayakuruhusiwa tena kukutana, kuweka mapadri wala kueneza mafundisho yao.[3] Theodosius alikataza wazushi wasiishi tena Konstantinopoli, na miaka 392-394 alitaifisha maabadi yao.[4]

Baada yake wanae wawili walishiriki utawala, Honorius upande wa Magharibi, na Arcadius upande wa Mashariki.

Waorthodoksi wanamheshimu kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Januari.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1.  "Theodosius I". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  2. Boyd (1905), p. 45
  3. Boyd (1905), p. 47
  4. Boyd (1905), p. 50
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Roma bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Theodosius Mkuu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.