Lango:Kenya
Lango hili lipo katika ujenzi
Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia WikiLango KenyaJamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi). Mji mkuu ni Nairobi. Mji mkuu ni Nairobi. Idadi ya watu imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kufikia milioni 50. Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi maelfu ya wanyama pori wa kila aina. Jina Kenya linatokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika, Kabla ya mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya liliitwa Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki, kwa hivyo hapakuwa na haja kutaja neno mlima uliporejelea mlima huo. Makala iliyochuguliwaNairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mmojawapo wa mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Afrika. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295. Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika. Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkare nairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi." Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng. (Soma zaidi...) Picha iliyochaguliwaJe wajua ...Wasifu uliochaguliwaDedan Kimathi (31 Oktoba 1920 – 18 Februari 1957) alikua Mkenya aliyeongoza harakati za kundi la Mau Mau za kutwaa ardhi iliyokuwa iko mikononi mwa wakoloni toka Uingereza. Kimathi alihukumiwa na kunyongwa kutokana na harakati zake za kuikomboa nchi ya Kenya. Waingereza, Serekali ya wakoloni ilimchukua Kimathi kama mgaidi, lakini wananchi wengi wa kabila la Gikuyu walimchukua Kimathi kama mpigania uhuru. Alizaliwa mnamo 31 Oktoba 1920 katika kijiji cha Thenge huko tarafa ya Tetu, wilaya ya Nyeri na alinyongwa na Waingereza tarehe 18 Februari 1957. JamiiMasomo inayohusu KenyaMilango inayohusianaAssociated Wikimedia |