Lango:Cote d'Ivoire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Coat of arms of Ivory Coast.svg

Karibu!!!
Welcome
BandeauportailCi2.jpg

Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

Lango la Cote d'Ivoire

Location on the world map
Cote d'Ivoire (tamka: kot divwar; kifar.: "Pwani la pembe za ndovu") (Kisw. pia: Kodivaa, Ivory Coast), kwa Kiingereza Ivory Coast ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana kwenye mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini.

Iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha zimeharibika kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Jamii

Wasifu Uliochaguliwa

Kolo Toure 8932.JPG

Kolo Habib Toure (alizaliwa mnamo 19 Machi 1981) ni mchezaji kandanda ambaye kwa sasa anaichezea, na ni nahodha wa Manchester City,ambayo ni klabu katika ligi kuu ya Uingereza na huichezea timu ya taifa ya Ivory Coast. Touré ni mchezaji wa kati wa safu ya ulinzi, yaani difenda, na anajulikana kwa kasi yake, nguvu yake na uanaspoti wake. Yeye ni kaka mkubwa wa Yaya Toure, mchezaji wa kuingo cha kati katika klabu ya Barcelona na Ibrahim Touré wa klabu ya Al-Ittihad.

Alizaliwa katika sehemu ya Bouaké, na baada ya jaribio wa muda mfupi, Toure alijiunga na Arsenal mnamo Februari 2002 kutoka ASEC Mimosas kwa paundi £ 150,000. Alipata kibali cha kazi cha Uingereza kutokana na status yake ya kuwa mchezaji wa kimataifa aliyekamilika. Awali alichezeshwa kama mchezaji wa kiungo cha kati wa kushambulia au kama mshambuliaji. Toure hakuichezea timu ya kwanza ya Arsenal hadi msimu uliofuata, dhidi ya Liverpool katika FA Community Shield mwezi Agosti mwaka wa 2002.


Mradi

Makala iliyochaguliwa

Regions of Côte d'Ivoire numbered (new 2011 regions).png

Mikoa ya Cote d’Ivoire (kwa Kifaransa: Régions de Côte d’Ivoire) ni ngazi ya pili ya ugatuzi nchini Cote d'Ivoire. Nchi imegawanywa katika wilaya 14 ambazo ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi. Wilaya mbili ni miji iliyoandaliwa kama wilaya huru na wilaya 12 za kawaida zinagawanyika katika mikoa 31.

Mikoa na wilaya zisizo huru, imegawanywa katika tarafa 108 ambazo ni ngazi ya tatu ya ugatuzi.


Picha Iliyochaguliwa

DesireTagro.jpg

Desire Tagro Asségnini (27 Januari 1959 - 12 Aprili 2011), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Cote d'Ivoire 2007-2010.


Je, wajua...?

  • ... kwamba Cote d'Ivoire iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha kwa jumla vimeharibika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe (2002-2011)?
  • ... kwamba lugha zinazotumika kwa kawaida nchini Cote d'Ivoire ni 65, lakini lugha rasmi ni Kifaransa?
  • ... kwamba Katika Cote d'Ivoire, Uislamu una 38.6%, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki) 32.8%, na dini asilia za Kiafrika 28%?