Lango:Cote d'Ivoire/Wasifu uliochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Orodha ya wasifu Uliochaguliwa[hariri chanzo]

  • Januari : Didier Drogba
  • Februari : Gervais Yao Kouassi
  • Machi : Kolo Toure
  • Aprili : Didier Zokora
  • Mei : Bernard Dadié
  • Juni :Josué Guébo
  • Julai : Alpha Blondy
  • Agosti : Didier Drogba
  • Septemba : Gervais Yao Kouassi
  • Oktoba : Kolo Toure
  • Novemba : Didier Zokora
  • Desemba : Bernard Dadié

Wasifu Uliochaguliwa, Aprili[hariri chanzo]

Alain Didier Zokora Deguy (amezaliwa 14 Desemba 1980 katika mji mkuu wa Abidjan) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Cote d'Ivoire (Ivory Coast), ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya huko Hispania, maarufu ya Sevilla FC na pia timu ya taifa ya Cote d'Ivoire. Zokora nikiungo muhimu katika klabu yake na timu yake ya taifa ya Cote d'Ivoire,yeye ni mchezaji mzuri wa katikati ambae anatumia ufundi wa hali ya juu katika uchezaji wake na amezungumziwa na wafatilia mpira wa miguu wengi kua ni mchezaji ambae anatumia akili na mbinu katika uchezaji wake.

Zokora alianza kucheza mpira katika katika ujana wake katika klabu ya ASEC Mimosas(Cote d'Ivoire) mwaka 1999/2000, huo mwaka alionekana ni miongoni mwa wachezaji wazuri katika klabu yake hiyo ya ASEC,basi baadhi ya klabu za Ulaya zilipendelea kumnunua, katika mwaka 2000 klabu ya Ubelgiji ya KRC Genk iliweza kupata fursa yakumnunua,Zokora alicheza katika klabu hiyo hadi mwaka 2004 na aliichezea klabu hiyo katika mechi 126 na alifunga goli li moja tu,nakuanzia mwaka 2004 alijiunga na klabu mashuhuri ufaransa ya Saint-Étienne huko ndipo alianza kuonekana kua nyota au kua mashuhuri katika ulimwengu wa mpira maana uchezaji wake katika timu hiyo ya Ufaransa ulikua mzuri sana na katika timu yake ya taifa maana alisaidia timu yake kushika nafasi za mwanzo katika Ligue 1(Ligi ya kwanza) ya Ufaransa