Nenda kwa yaliyomo

Didier Zokora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Didier Zokora
Maelezo binafsi
Jina kamili Alain Didier Zokora Deguy
Tarehe ya kuzaliwa 14 Desemba 1980 (1980-12-14) (umri 43)
Mahala pa kuzaliwa    Abidjan, Cote d'Ivoire
Urefu mita 1.80
Nafasi anayochezea Katikati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Trabzonspor
Namba 15
Klabu za vijana
ASEC Mimosas
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2009 Trabzonspor
Timu ya taifa
2000 Cote d'Ivoire

* Magoli alioshinda

Alain Didier Zokora Deguy (amezaliwa 14 Desemba 1980 katika mji mkuu wa Abidjan) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Cote d'Ivoire (Ivory Coast), ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya huko Hispania, maarufu ya Sevilla FC na pia timu ya taifa ya Cote d'Ivoire.

Masuala ya mpira

[hariri | hariri chanzo]

Namna ya uchezaji wake

[hariri | hariri chanzo]

Zokora nikiungo muhimu katika klabu yake na timu yake ya taifa ya Cote d'Ivoire,yeye ni mchezaji mzuri wa katikati ambae anatumia ufundi wa hali ya juu katika uchezaji wake na amezungumziwa na wafatilia mpira wa miguu wengi kua ni mchezaji ambae anatumia akili na mbinu katika uchezaji wake.

Kuanza kwake kucheza mpira

[hariri | hariri chanzo]
Zokora akicheza dhidi ya Arsenal katika mwezi wa Januari 2007.

Zokora alianza kucheza mpira katika katika ujana wake katika klabu ya ASEC Mimosas(Cote d'Ivoire) mwaka 1999/2000,huo mwaka alionekana ni miongoni mwa wachezaji wazuri katika klabu yake hiyo ya ASEC,basi baadhi ya klabu za Ulaya zilipendelea kumnunua,katika mwaka 2000 klabu ya Ubelgiji ya KRC Genk iliweza kupata fursa yakumnunua,Zokora alicheza katika klabu hiyo hadi mwaka 2004 na aliichezea klabu hiyo katika mechi 126 na alifunga goli li moja tu,nakuanzia mwaka 2004 alijiunga na klabu mashuhuri ufaransa ya Saint-Étienne huko ndipo alianza kuonekana kua nyota au kua mashuhuri katika ulimwengu wa mpira maana uchezaji wake katika timu hiyo ya Ufaransa ulikua mzuri sana na katika timu yake ya taifa maana alisaidia timu yake kushika nafasi za mwanzo katika Ligue 1(Ligi ya kwanza) ya Ufaransa na alichezea klabu hiyo ya ufaransa mechi 66 na alifunga magoli mawili tu,Uchezaji wake mzuri ulipeleka klabu nyingi kubwa kubwa barani Ulaya kupendelea kumnunua lakini klabu ya Uingereza iliweza kumnunua kwani ilitoa pesa nyingi na ilikua mwaka 2006 na aliichezea klabu hiyo ya[[Uingereza kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2009.

Kutoka kwake Tottenham nakuelekea Sevilla

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2009 tar 8 Julai, klabu ya Tottenham ilikubali kumuuzisha mchezaji wake huyo muhimu kwenye klabu ya Sevilla ya Uhispania kiwango cha pesa hakikutangazwa,klabu hiyo inashiriki katika Ligi ya kwanza ya Uhispania

Kuanza kwake kucheza katika timu ya taifa

[hariri | hariri chanzo]

Zokora alianza kuichezea timu yake ya taifa ya Cote d'Ivoire mwaka 2000 lakini bila kua kiungo muhimu kutokana na umri wake mdogo nakuchezea katika ligi ya nyumbani kwani timu ya taifa ya Cote d'Ivoire hutegemea zaidi wachezaji wanaocheza nje, alipotoka nakujiunga na klabu ya huko Ubelgiji ndio alianza kucheza vizuri katika timu ya taifa nakushiriki katika mechi nyingi kama kiungo muhimu lakini alidhihirika zaidi nakupata umashuhuri zaidi mwaka 2005 katika mashindano yakugombea tiketi yakuelekea katika kombe la dunia lililofanyika huko Ujerumani waliweza kunyakua tiketi kutoka katika mikono ya timu kali kama Misri na Kameruni na huo mwaka waliweza kuifunga Misri nyumbani Misri 2-1 na huko Cote d'Ivoire 2-0 timu Cote d'Ivoire huo mwaka ilionekana timu kali sana ambayo ni vigumu kufungwa kiuraisi ilishiriki katika kombe la Mataifa ya Afrika misri ilitoa timu nyingi kama Nigeria na Kameruni, walifika fainali lakini walifungwa kwa mapenelti na waandalizi wa kombe hilo Misri.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Didier Zokora kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.