Elimu nchini Cote d'Ivoire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Watoto darasani huko mjini Abidjan

Elimu nchini Côte d'Ivoire inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi. Kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kwa watu wazima bado kipo chini: mnamo 2000, ilikadiriwa kwamba 48.7% ya jumla ya wakazi wanajua kusoma na kuandika (60.8% ya wanaume na 38.6% ya wasichana). [1] Watoto waliowengi kati ya miaka 6 na 10 hawajaandikishwa shule. [2] Idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya sekondari ni wanaume.[3] Mwishoni mwa elimu ya sekondari, wanafunzi wanakaa na kufanya mtihani wa mwisho (Baccalauréat).[3] Nchi ina vyuo vikuu mjini Abidjan (Université de Cocody) na huko Bouaké, (Université de Bouaké).

Mfumo wa elimu[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa elimu yao umegawanyika katika hatua tatu: shule ya msingi hudumu kwa miaka sita, inapelekea kupata cheti cha masomo ya msingi; shule ya secondari hudumu kwa miaka saba, inapelekea kupata cheti kuhitimu masomo hayo. Elimu ya chuo kikuu, inapatikana mjini Abidjan tu, katika kilele cha shahada. Idadi kubwa ya taasisi za masuala ya kiufundi na mafunzo wa ualimu nayo hutolewa baada ya elimu ya msingi na sekondari pia. Kulikuwa hakuna mfumo wa elimu ya watu wazima, ijapokuwa watu wazima wengi huudhuria kozi mbalimbali nyakati za usiku, katika maeneo ya vijijini, wanapata elimu yao ya kujua kusoma na kuandika na maelekezo mengine kwa kupitia redio.

Mashulu mengi ya umma yalikuwa yakitoa ukufunzi bure, ijapokuwa wanafunzi hulipa ada ya kiingilio cha awali na kununua sare. Huduma nyingi ilikuwa bure, na baadhi ya wanafunzi wanapata udhamini na serikali, kikawaida hufanya mrejesho kwa kuwapa ajira serikalini baada ya kuhitimu.

Makadiro yaliyofanywa mwaka wa 1980 inaonesha kwamba asilimia 14 ya mshule ya msingi na asilimia 29 ya mashule yasekondari yalikuwa ya watu binafsi. Mengi yao yalikuwa mashule ya Katoliki, iliyokuwa ikifanyiwa kazi na walimu wa kidini na walimu wa kawaida, na sehemu ya mshahara inatolewa ruzuku kutoka serikalini.

Mashule ya Wakatoliki yalikuwa yakifanya kazi zake mjini kusini na mshariki, lakini pia yalikuwa yakipatikana huko sehemu zingine za nchi. Mafunzo ya kidini yalikuwa hayaruhusiwi katika mashule ya serikali. Mashule ya Kiislamu yalikuwa maarufu huko mjini kaskazini na yalikuwa huru, lakini yalikuwa hayaungwi mkono na serikali. Baadhi ya wanafunzi huudhuria mashule yote ya Kiislamu na umma vilevile.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/fields/2103.html
  2. Earthtrends.wri.org (PDF). Iliwekwa mnamo 2010-12-06.
  3. 3.0 3.1 Côte d'Ivoire – Secondary Education. Education.stateuniversity.com. Iliwekwa mnamo 2010-06-20.