Nenda kwa yaliyomo

Elimu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Darasa huko mjini Sam Ouandja, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Elimu ya umma katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni bure, na elimu ni kiada kuanzia umri kati ya miaka 6 hadi 14.[1] Vifo vinavyotokana na UKIMWI - vimechukua nafasi kubwa sana kwa walimu, hilo limepelekea kufungwa kwa shule za msingi zaidi ya 100 kati ya mwaka 1996 na 1998.[1]

Mwaka wa 1991, idadi kamili ya waliojiandikisha kwa ajili ya elimu ya msingi ilikuwa asilimia 56.9. Mwaka wa 2000, idadi kamili ya watoto wenye umri kati ya 6 hadi 11 walioandikishwa kwa ajili ya elimu ya msingi ilikuwa asilimia 43 pekee. Ripoti ya idadi ya mahudhurio kwa ajili ya elimu ya msingi haikupatikana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mwaka wa elimu 2001. Idadi ya uandikishwaji haifanani na mahudhurio ya wanafunzi mashuleni.

Hakuna fursa sawa kielimu kwa watoto wa kike. Kwa mwaka wa kwanza wa masomo,asilimia 65 ya wasichana waliandikishwa katika elimu ya msingi. Lakini hali hii imeporomoka hadi kufikia asilimia 23 kwa wasichana baada ya miaka sita ya elimu ya msingi na hiyo ilikuwa kwa mwaka wa 2007. Wasichana wengi wanaacha shule wakiwa na umri mdogo aidha kwa tamaa au msukumo kutoka katika familia ili aweze kuoelewa na kupata watoto.[2]

Bajeti ndogo inayotengwa kwa ajili ya elimu na tabia ya kutolipa mishahara kwa wakati umepelekea kuwa na upungufu wa walimu na hivyo basi hali hiyo inaongeza idadi ya watoto wa mitaani. Bajeti ya taifa inayotolewa na serikali inakidhi kwa asilimia 12 tu, iliongezwa hadi kufikia walau asilimia 18 katika miaka ya 1990. Kulingana na serikali, walisema itapanda hadi kufikia asilimia 25 ifikapo mwaka wa 2010.

Kulikuwa na wanafunzi wapatao 800,000 ambao waliathiriwa na machafuko yaliyotokea mwezi wa Desemba 2012 kutokana na uasi wa Séléka. Walimu wengi waliomba hifadhi ya kivita bado hawajarudi nchini humo.

Idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika nchini humo kati ya watu wazima na vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 imefikia asilimia 72.3, kwa umri huohuo lakini upande wa kina mama kiwango chao ni asilimia 59.1.[3]

  1. 1.0 1.1 "Central African Republic". 26 Desemba 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Desemba 2014. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2015. {{cite web}}: |archive-date= / |archive-url= timestamp mismatch; 18 Desemba 2013 suggested (help)CS1 maint: date auto-translated (link) Findings on the Worst Forms of Child Labor (2001). Bureau of International Labor Affairs, U.S. Department of Labor (2002). This article incorporates text from this source, which is in the public domain.
  2. "CENTRAL AFRICAN REPUBLIC 2013 HUMAN RIGHTS REPORT" (PDF). U.S. Department of State. Iliwekwa mnamo Novemba 14, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Statistics". Unicef. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-01. Iliwekwa mnamo Novemba 14, 2016. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)