George W. Bush
George W. Bush | |
Rais Bush, mnamo 2003 | |
Rais wa Marekani
| |
Aliingia ofisini Januari 20, 2001 | |
Makamu wa Rais | Dick Cheney |
---|---|
mtangulizi | Bill Clinton |
aliyemfuata | Barack Obama |
tarehe ya kuzaliwa | 6 Julai 1946 |
utaifa | American |
chama | Republican |
ndoa | Laura Welch (m. 1977–present) |
watoto | Barbara Bush (b. 1981) Jenna Bush |
signature | |
tovuti | http://www.georgewbush.com |
George Walker Bush ( /ˈdʒɔrdʒ ˈwɔːkər ˈbʊʃ/ (info), alizaliwa 6 Julai 1946) alikuwa rais wa Marekani tangu mwaka 2001 mpaka mwaka 2009. Yeye ni mwenyeji wa jimbo la Texas alipokuwa gavana kabla ya kugombea urais.
George W. Bush ni mwana wa rais George H. Bush aliyetawala Marekani kati ya miaka 1989 - 1993. George W. amemwoa Laura Bush wana mabinti mawili.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Bush alizaliwa katika jimbo la Connecticut akafuata elimu yake hadi chuo kikuu cha Yale. Hakushiriki katika vita ya Vietnam lakini alijiandikisha kati ya wanamgambo wa jimbo la Texas.
Mwaka 2000 aligombea urais kwa chama cha Republican. Alishinda kufuatana na azimio la mahakama kuu kwa sababu kura ya jimbo la Florida haikueleweka vizuri na kwa jumla kura zake zilikuwa karibu sawa na zile za mpinzani wake Al Gore.
Mwaka 2004 Bush alirudishwa kama rais kwa awamu ya pili na ya mwisho.
Vipindi viwili vya Bush viliathiriwa sana na mashambulio ya 11 Septemba 2001. Baada ya shambulio hilo la Al Qaida Bush aliamuru vita dhidi ya Afghanistan ambako wagaidi wa Al Qaida walikuwa na kimbilio.
Mwaka uliofuata Bush aliuamua kwa sababu zisizoeleweka vema kushambulia pia Iraq ingawa Iraq haikushiriki katika mashambulio ya 11 Septemba wala kuwa na uhusiano na Al Qaida.
Mwanzoni Marekani pamoja namsaada wa Uingereza ilifaulu vema kushinda jeshi la Iraq na kumpindua dikteta Saddam Hussein. Lakini ushindi huu uligeukia kuwa vita ndefu ya wanamgambo wa Iraqi dhidi ya Marekani. Watu wengi waliendelea kufa na vita hii ya kuendelea iliharibu sifa za Bush.
}}