Nenda kwa yaliyomo

James Buchanan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
James Buchanan

Muda wa Utawala
Machi 4, 1857  Machi 4, 1861
Makamu wa Rais John C. Breckinridge
mtangulizi Franklin Pierce
aliyemfuata Abraham Lincoln

tarehe ya kuzaliwa (1791-04-23)Aprili 23, 1791
Cove Gap, Pennsylvania, Marekani
tarehe ya kufa 1 Juni 1868 (umri 77)
Lancaster, Pennsylvania, Marekani
mahali pa kuzikiwa Woodward Hill Cemetery
utaifa Democratic
mhitimu wa Dickinson College (Bachelor of Arts)
signature
tovuti Makumbusho ya (Wheatland)

James Buchanan Jr (23 Aprili 17911 Juni 1868) alikuwa Rais wa 15 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1857 hadi 1861. Kaimu Rais wake alikuwa John Breckinridge.

Alishika nyadhifa ya Urais kuanzia mwaka 1857 hadi 1861. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuanzia 1845 hadi 1849 na aliwakilisha Pennsylvania katika mabaraza yote mawili ya Bunge la Marekani[1]. Buchanan alikuwa mtetezi wa haki za majimbo, hasa kuhusu suala la utumwa, na alipunguza jukumu la serikali ya shirikisho kabla ya kuzuka kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani[2]. Buchanan alikuwa wakili huko Pennsylvania na alishinda uchaguzi wake wa kwanza kuingia katika Baraza la Wawakilishi la jimbo kupitia Chama cha Federalist. Alichaguliwa katika Baraza la Wawakilishi la Marekani mwaka 1820 na alihudumu kwa mihula mitano, akijiunga na Chama cha Democrat cha Andrew Jackson. Mnamo 1832, aliteuliwa kuwa balozi wa Marekani nchini Urusi.

Mnamo 1834 alichaguliwa kuwa seneta wa Marekani kutoka Pennsylvania, nafasi aliyoshikilia kwa miaka 11.Mnamo 1845, Rais James K. Polk alimteua kuwa waziri wa mambo ya nje, na mwaka 1853 alitumwa na Rais Franklin Pierce kuwa balozi wa Marekani nchini Uingereza.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Buchanan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.