Nenda kwa yaliyomo

John Breckinridge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John C. Breckinridge

John Cabell Breckinridge (21 Januari 182117 Mei 1875) alikuwa mwanasheria, mwanajeshi na mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia. Alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais James Buchanan kuanzia mwaka wa 1857 hadi 1861. Baada ya ushindi wa Abraham Lincoln mwaka wa 1860, Breckinridge akawa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Kentucky kwa miezi michache tu. Baada ya majimbo saba kuasi na baada ya kuanzishwa kwa vita, Breckinridge akafukuzwa kutoka senati akakimbilia Kusini na kuwa mwanajeshi upande wa majimbo maasi. Baada ya Kusini kushindwa vitani, Breckinridge akawa mkimbizi katika nchi za Kuba, Uingereza na Kanada. Mwaka wa 1868 akaruhusiwa kurudi Marekani lakini hakuingia mambo ya siasa tena. Akafariki mwaka wa 1875 akiwa na umri wa miaka 54 tu baada ya upasuaji kwa ajili ya kutibu majeraha aliyoyapata vitani.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Breckinridge kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.