Nenda kwa yaliyomo

Ganimedi (mwezi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ganimedi (Mshtarii))
Ganimedi

Ganimedi (ing. Ganymede) ni mwezi mkubwa zaidi wa Mshtarii (Jupiter) ambayo ni sayari ya tano kutoka kwa Jua na sayari kubwa katika mfumo wa Jua. Ni pia mwezi mkubwa katika mfumo wa Jua.

Kipenyo cha Ganimedi ni kilomita 5262 km hivyo ni kubwa kuliko sayari ya kwanza Utaridi (Mercury). Lakini ina nusu ya masi yake tu maana haina kiasi hiki cha densiti.

Kati ya miezi ya Mshtarii, Ganimedi iko kwenye nafasi ya saba ukihesabu kutoka sayari yenyewe.

Ganimedi inazunguka Mshtarii katika kipindi cha siku saba hivi. Obiti yake inashikamana na obiti za miezi Europa na Io katika uhusiano wa 1: 2: 4.

Ugunduzi na Jina

[hariri | hariri chanzo]

Ganimedi ni mmoja wa miezi ya Mshtarii iliyotambuliwa mnamo 7 Januari 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa mtu wa kwanza kutazama nyota kwa kutumia darubini. Hivyo inajulikana pia kama mwoja wa "miezi ya Galileo" maana iligunduliwa na Galilei pamoja na miezi 3 mingine ya Mshtarii na hayo yalikuwa magimba ya kwamnza yaliyoonekana kuzunguka sayari nyingine.[1]

Iliwahi kuitwa kwa majina mbalimbali. Jina lililobaki lilipendekezwa na mwanaastronomia Simon Marius. Kufuatana na desturi ya Ulaya kuziita sayari kwa majina ya miungu kutoka dini za kale, Marius alipendekeza jina la "Ganimedi" (gir. Γανυμήδης ganimedes) , kijana mpenzi wa mungu mkuu Zeu (sawa na Jupiter wa Waroma wa Kale) katika masimulizi ya Wagiriki. wa Jupita).

Muundo na tabia zinazojulikana

[hariri | hariri chanzo]
Muundo wa kudhaniwa wa Ganimedi kufuatana na data zilizopatikana hadi 2020

Kwenye kitovu chake kuna kiini cha metali kinachofikiriwa kuwa katika hali ya joto na kiowevu ambacho ni hasa chuma na nikeli. Myuko :en:convection ndani ya kiini hiki ni sababu ya kumkinika ya ugasumaku wake. Ganimedi hadi sasa ni mwezi wa pekee uliogunduliwa kuwa na ugasumaku.

Ganymede inadhaniwa imeundwa na miamba ya kisilika na maji. Uso wake wa miamba hufunikwa na bahari yenye kina cha kilomita mia kadhaa. Tabaka la juu la bahari hiyo limeganda, ni barafu. Kwa hiyo uso wote wa Ganimedi ni barafu[2]. Kuna makadirio ya kwamba kiasi cha maji kwenye Ganimedi kinazidi jumla ya maji Duniani.[3]

Uso unaonyesha maeneo meusi na maeneo meupemeupe. Sehemu nyeusi zinaonyesha kasoko nyingi kutokana na migongano na asteroidi ndogo, sehemu nyeupe zinaonyesha zaidi mabonde na safu za milima. Inadhaniwa kwamba sehemu nyesui ni za kale zaidi, na sehemu nyeupe zimepokea umbo kutokana na miendo ya gandunia .

Ugasumaku wa Ganimedi inadhaniwa umetokana na myuko (en:convection) ndani ya kiini chake cha chuma moto katika hali ya kiowevu[4].

Ganimedi ina angahewa hafifu sana ya inayonyesha oksijeni ambayo ni pamoja na O, O 2, na labda O 3 ( ozoni ). Viwangi vidogo vya hidrojeni vilipimwa pia kwwa njia ya uchambuzi wa spektra.

Uchunguzi

[hariri | hariri chanzo]
Picha iliyotumwa na Mariner 10 kwenye mwaka 1973

Mbali na kuiangalia kwa darubini, vipimaanga kadhaa waliongeza data na elimu kuhusu Ganimedi. Hadi sasa vyote vilitumwa na NASA ya Marekani:

  • Pioneer 10 ilipita kwa Ganimedi mwaka 1973 ikatuma picha ya kwanza ya mwezi huo ikafuatwa na Pioneer 11 mwaka 1974[5].
  • Voyager 1 na Voyager 2 vilifuata mwaka 1979. Viliweza kupima ukubwa wa Ganimedi vikatambua kuwepo kwa mabonde na milima

[6].

  • Galileo ilifika mwaka 1995 ilizunguka Mshtarii na miezi yake kwa miaka nane. Galileo ilipita mara kadhaa karibu na Ganimedi, safari moja kilomita 260 pekee juu ya uso wake. Iligundua ugasumaku na bahari ya maji iliyopo chini ya uso wa barafu[7]

+ New Horizons ilipita mwaka 2007[8]

Kipimaanga kinachopangwa kufuata ni JUICE (Jupiter Icy Moon Explorer) inayoandaliwa na mamlaka ya usafiri wa anga ya Ulaya ESA. Ilitarajiwa kurushwa mwaka 2022. Itahitaji zaidi ya miaka 7 kufika kwenye mfumo wa Mshtarii, itatangulia kupita kwenye miezi ya Europa na Kallisto hadi kuingia katika obiti ya kuzunguka Ganimedi mnamo mwaka 2032[9].

Ulinganishi wa ukubwa wa Dunia (kulia), Mwezi (juu), na Ganimedi (chini).
  1. "Ganymede (satellite of Jupiter)". Encyclopædia Britannica. https://www.britannica.com/place/Ganymede-satellite-of-Jupiter. Retrieved November 19, 2019.
  2. NASA’s Hubble Observations Suggest Underground Ocean on Jupiter's Largest Moon, tovuti ya NASA tar. March 12, 2015, iliangaliwa Mei 2018
  3. Jupiter moon Ganymede could have ocean with more water than Earth – NASA Archived 5 Oktoba 2018 at the Wayback Machine., tovuti ya Russia Today ya 13 Mar, 2015, iliangaliwa Mei 2018
  4. Volwerk, M.; Kivelson, M.G.; Khurana, K.K.; McPherron, R.L. (1999). "Probing Ganymede's magnetosphere with field line resonances" (PDF). J. Geophys. Res. 104 (A7): 14, 729–14, 738. Bibcode:1999JGR...10414729V. doi:10.1029/1999JA900161. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2009-03-27. Iliwekwa mnamo 2021-03-16. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  5. "Pioneer 11". Solar System Exploration. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 2, 2011. Iliwekwa mnamo Januari 6, 2008. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20110902202131/http://sse.jpl.nasa.gov/missions/profile.cfm?Sort= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "The Voyager Planetary Mission". Views of the Solar System. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 3, 2008. Iliwekwa mnamo Januari 6, 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. McCord, T.B.; Hansen, G.V.; na wenz. (1998). "Non-water-ice constituents in the surface material of the icy Galilelean satellites from Galileo near-infrared mapping spectrometer investigation". J. Geophys. Res. 103 (E4): 8, 603–8, 626. Bibcode:1998JGR...103.8603M. doi:10.1029/98JE00788.
  8. "Pluto-Bound New Horizons Spacecraft Gets A Boost From Jupiter". Space Daily. Iliwekwa mnamo Januari 6, 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Dougherty; Grasset (2011). "Jupiter Icy Moon Explorer". http://www.lpi.usra.edu/opag/Oct2011/presentations/Dougherty.pdf. Parent page: OPAG October 2011 Presentations

 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: