Fransiska wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
AntoniazzoRomano.jpg

Fransiska wa Roma (kwa Kiitalia Francesca Romana; 13849 Machi 1440) alikuwa mtawa kutoka Roma, Italia.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa Paulo V kuwa mtakatifu kuanzia mwaka wa 1608.

Tarehe ya kifo chake, yaani 9 Machi ndiyo sikukuu yake[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Fransiska alizaliwa katika mji wa Roma, Italia, mwaka 1384. Aliolewa mwaka 1396, akazaa watoto watatu.

Aliishi wakati mgumu, hata hivyo aliwapatia maskini mali yake, na akawauguza wagonjwa. Alijulikana sana kwa upole, uvumilivu na kujitoa kwake mhanga kuwasaidia maskini.

Mwaka 1425 alianzisha Shirika la Waoblati Wabenedikto, akifuata Kanuni ya Mt. Benedikto. Alifariki dunia mwaka 1440.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.