Alda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Alda wa Siena (kwa Kiitalia Aldobrandesca pia; 1249 hivi – 1309 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo wa Italia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Aprili.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alda alizaliwa Siena (leo mkoani Toscana); baada ya kuishi miaka saba katika ndoa bila kupata mtoto, alifiwa mumewe.

Hapo alitawa upwekeni nje ya mji na kujitosa katika kujinyima na kutoa sadaka.

Baada ya kupata njozi kuhusu Yesu kutenda kama inavyoelezwa na Injili, aligawa mali zake zote akaenda kuishi hospitalini ili kuhudumia wagonjwa. Katika kazi hiyo ilitokea miujiza kadhaa.

Siku moja wahudumu wenzake wasioamini njozi zake, alipokuwa nje ya nafsi yake, walimchoma mwilini kwa sindano na moto, lakini hakuwa na itikio lolote mpaka baada ya kujirudia. Hapo alisema tu kwa unyenyekevu, "Mungu awasamehe", jambo lililomvutia wote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Dictionary of Saints, by John Delaney

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.