Nenda kwa yaliyomo

Akon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akon

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Aliaune Badara Akon Thiam
Amezaliwa 30 Aprili 1973 (1973-04-30) (umri 51)
Asili yake Dakar, Senegal
Aina ya muziki Hip hop, R&B, Pop
Kazi yake Mwanamuziki
Mtayarishaji
Mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi 1996–hadi leo
Studio Universal, Akonik, SRC, Konvict Muzik, UpFront
Ame/Wameshirikiana na DJ Khaled, Lil Wayne, Colby O'Donis, Kardinal Offishall, Snoop Dogg, T-Pain, Young Jeezy
Tovuti www.akononline.com


Aliuane Badara Akon Thiam (anafahamika zaidi kwa jina lake la kati ambalo analitumia kwa usanii; amezaliwa 30 Aprili 1973[1][2]) ni chotara wa Msenegali na Mmarekani ambaye ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za R & B, mtayarishaji wa rekodi, mfanyabiashara, na mhisani.

Alipata umashuhuri mwaka wa 2004 kufuatia kutolewa kwa wimbo wa "Locked Up", uliokuwa wa kwanza kutoka albamu yake ya kwanza iliyoitwa, Trouble.

Albamu yake ya pili, Konvicted, ilimwezesha kuteuliwa kushindania tuzo la Grammy kutokana na wimbo wa "Smack That". Yeye kufikia sasa ameanzisha kampuni mbili za kurekodi ambazo ni, Konvict Muzik na Kon Live Distribution.

Yeye anajulikana kama mojawapo wa waimbaji waliofanikiwa na hodari zaidi wa mtindo wa R & B wa karne ya 21, apataye zaidi ya dola milioni 30 kwa mwaka. Haya ni kulingana na jarida la Forbes.

Akon mara nyingi hushirikiana na wasanii wengine na kwa sasa ameshirikishwa katika zaidi ya nyimbo 200 na ana nyimbo 36 kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri. Yeye ni msanii wa kwanza kuchukua nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia, kwa mara mbili, kwenye chati za Mabango ya nyimbo 100 mashuhuri. Yeye ameteuliwa mara 6 kushindania tuzo ya Grammy na amehusika katika utayarisha ji wa nyimbo za wasanii kama vile Lady Gaga, T-Pain, Leona Lewis miongoni mwa wengine. Yeye amekuwa na nyimbo 19 kwenye kitengo cha nyimbo 20 bora duniani kote.

Akon amedai katika mahojiano kwamba jina lake kamili ni Aliuane Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam [3] ingawa kuna utata na mjadala kuhusu jina lake halisi na tarehe yake ya kuzaliwa. Akon kwa kawaida anajulikana kama Aliuane Thiam. Juu ya jina lake refu , jina kamili la Akon limeripotiwa kuwa Aliaune Badara Thiam na Alioune Badara Thiam na mtandao wa About.com unadai kwamba jina lake la katikati halijawahi kuthibitishwa. Kuhusu tarehe yake ya kuzaliwa, baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba Akon alizaliwa mwaka 1981. Taasisi zingine, ikiwemo AP, wanadai kuwa Akon alizaliwa mwaka wa 1973, na mamake alisaidiwa kujifungua na daktari msenegali aitwaye Magueye Seck.

Hati za kisheria zilizotolewa na The Smoking Gun zinaonyesha jina la Akon kama Aliuane Damala Thiam na tarehe yake ya kuzaliwa kama 1973/04/30 [4] au 1973/04/16,[5] hata hivyo shirika la BBC linasema kuwa Akon alizaliwa tarehe 14 Oktoba 1981.

Maisha ya utotoni

[hariri | hariri chanzo]

Akiwa mwanawe mcheza ala za muziki aliyesifika kutoka Senegali aliyejulikana kama Mor Thiam, Akon alikulia katika mandhari ya muziki na alifundishwa kucheza ala kadhaa ikiwemo djembe. Yeye alizaliwa St Louis, Missouri, USA ili kukwepa shughuli za kutafuta kibali cha uhamiaji, lakini aliishi mjini Dakar, Senegal hadi alipofikisha umri wa miaka 7, kisha akabadilishana kati ya kuishi Senegali na Marekani hadi alipofikisha umri wa miaka 15, alipohamia kabisa mjini Jersey, New Jersey.

Wakati Akon aliposemaka kuwa katika jela kwa miaka 3, alianza kutambua kipawa chake cha muziki na akaanza kujivunia historia ya muziki iliyokuwa kwenye familia yake. Mchanganyiko wake wa kipekee wa mtindo wa Afrika Magharibi, ujuzi wake na hatimaye mitindo yake ya densi iliwavutia wakuu wa shirika la Universal. Akon alianza kuandika na kurekodi nyimbo katika studio yake ya nyumbani. Tepu zake zilifika kwenye kampuni hiyo ya SRC/Universal, ambayo ilitoa albumu (LP) yake ya kwanza, Trouble, mnamo juni 2004. Albamu hii ni mseto wa mtindo mwororo wa Akon wa Afrika Magharibi Ukichanganywa na MIDU kutoka Pwani ya Mashariki na Kusini. Nyimbo nyingi za Akon huanza kwa sauti ya kufunguka kwa mlango wa jela naye akitamka neno "Konvict".

Maisha ya binafsi na madai

[hariri | hariri chanzo]

Akon ni Mwislamu, na anasema hajawahi kulewa pombe kutokana na imani yake. Kumekuwa na madai kuwa ana wake watatu, hata hivyo amebaini kuwa anaye mmoja tu, aitwaye Tomeka. Akon alidai kuwa amepata watoto sita na wanawake watatu tofauti katika mahojiano na jarida la Blender. Akon pia anadai kuwa na uhusiano mzuri sana na watoto wake wote, na kwamba yeye anataka kukinga familia yake kutokana na jicho la umma. Yeye pia anasema kwamba dini yake ilimfanya kuwa mtu bora, na inampa mwongozo wa jinsi ya kutagusana na watu wengine maishani.

Yeye pia ana shirika lake la kutoa msaada kwa watoto wasiojiweza barani Afrika liitwalo Konfidence Foundation. Akon anamiliki mgodi wa almasi katika Afrika ya Kusini na anakanusha uwepo wa almasi za damu (zinajulikana pia kama " almasi za vita") akisema, "Hata siamini kuwa kuna almasi za vita. Hiyo ni filamu tu. Hebu fikiria. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kufikiria chochote kuhusu almasi ya vita hadi wakati filamu hii ilipotolewa. Hata hivyo,tangu wakati huo yeye amesema kuwa hakubali kwamba almasi za damu zipo, na kwamba anamiliki nusu ya mgodi mmoja uliopo Afrika ambao unatia jitihada kuepuka matumizi ya almasi za damu huku wakizifaidi jamii zinazowazunguka. Inadaiwa kuwa aliwahi kushiriki katika ulanguzi wa madawa ya kulevya, lakini yeye amekanusha akisema hajawahi kutumia madawa haya, ingawa maneno ya baadhi ya nyimbo zake yanakinzana na makanusho yake.

Jarida la "The Smoking Gun" liliripoti, mnamo Aprili 2008, kwamba historia ya Akon ya kufungwa jela imeongezwa chumvi. Madai ya kuwa Akon alikuwa sehemu ya genge la wizi na kwamba alikaa miaka mitatu gerezani yalikabiliwa na rekodi za mahakama na za mahojiano na wachunguzi waliohusika katika kesi yake.

Kulingana na makala ya jarida la "Smoking Gun" , Akon hakushtakiwa na hatia yoyote ya uhalifu na hakutumikia kifungo chochote gerezani kati ya 1999-2002 kama alivyodai hapo awali. Yeye alisema kwamba jaribio la jarida la "The Smoking Gun" la kumharibia jina halina maana yoyote kwani hilo ni jambo analojaribu kulisahau." Akon alisema kuwa yeye hajawahi kukaa kwenye jela kipindi cha miaka 3 mfululizo, lakini amewahi kukaa vipindi vifupu vifupi ambavyo vimefikia miaka mitatu, na anasema kwamba huko ni kutoelewa kwa makala ya Smoking Gun. Japo ana historia ya uhalifu , Akon anatangaza kwamba amebadilisha mienendo ya maisha yake.

2004-05: Albamu ya kwanza: Trouble

[hariri | hariri chanzo]

Albamu yake ya kwanza, 'Trouble' ilitolewa Juni tarehe 29, 2004. Albamu hii ina nyimbo kama "Locked Up" na "Lonely", "Belly Dancer (Bananza)", "Pot of Gold", na "Ghetto." Albamu hii ndiyo iliyokuwa ya kwanza kutolewa na kampuni yake mpya ya kurekodi ya Konvict Music. Msukumo wa kuimba wimbo wake wa kwanza ulitokana na miaka mitatu aliyokaa kwenye jela kwa sababu ya 'kuiba'. Wimbo wa "Locked Up" uliorodheshwa kwa nyimbo 10 bora nchini Marekani na tano bora nchini Uingereza. "Wimbo wa "Ghetto" ulivuma kwenye redio wakati ulipochanaganywa upya na DJ Green Lantern na kujumuisha mistari kutoka wasanii 2Pac na The Notorious B.I.G.

Katika mwaka wa 2005, yeye alitoa wimbo "Lonely" (ambao ni sampuli ya wimbo wa Bobby Vinton wa "Mr Lonely"). Wimbo huo uliorodheshwa miongoni mwa nyimbo tano bora kwenye orodha ya Bango laynyimbo 100 mashuhuri, na ukaongoza kwenye chati katika nchi ya Australia, Uingereza na Ujerumani. Albamu yake pia ilifikia namba moja nchini Uingereza katika mwezi wa Aprili 2005. Wakati runinga ya muziki ya 'The Box' ilikuwa ikichagua nyimbo kumi bora za wiki , uchaguzi ambao ulikadiriwa kwa kiasi cha mara ambayo video hiyo iliombwa na mashabiki, wimbo wa Akon "Lonely" ndio ulioongoza kwenye chati hiyo kwa muda mrefu zaidi, kwani ulikaa wiki kumi na tano. Akon kisha alitoa wimbo, akishirikiana na msanii kutoka New Zealand aliyeitwa Savage, ulioitwa 'Moonshine', na ambao ulivuma huko New Zealand na Australia, na ukawa namba moja katika chati ya New Zealand. Katika mwaka wa 2005, alishiriki katika albamu ya kwanza ya mwimbaji Young Jeezy katika wimbo wa "Soul Survivor." Mwezi Desemba mwaka uo huo meneja wake, Robert Montanez aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya mzozo huko New Jersey.

2006-07: albamu ya Konvicted

[hariri | hariri chanzo]
Akon akicheza na Gwen Stefani katika The Sweet Escape Tour.

Albamu ya pili ya Akon, Konvicted ilitolewa tarehe 14 Novemba 2006. Ilikuwa na nyimbo alizoshirikisha waimbaji kama Eminem, Snoop Dogg na Styles P. Wimbo wa kwanza "Smack That" aliomshirikisha Eminem ulitolewa Agosti 2006 na ukashika nafasi ya pili kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri kwa wiki tano mfululizo. Wimbo wa "I Wanna Love You," (akimshirikisha Snoop Dogg) ndio uliokuwa wimbo wa pili uliotolewa Septemba, na ukawa ndio ambao ungekuwa wa kwanza wa Akon kuwa namba moja kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri, na wa pili wa Snoop. Wimbo huu wa "I Wanna Love You" uliongoza kwenye chati za Marekani kwa muda wa wiki mbili mfululizo. Katika Januari 2007, wimbo wa tatu "Don't Matter" ambao ulikuwa wimbo wa kwanza, alioimba bila kumshirikisha yeyote, kuwa namba moja, na wimbo wake wa pili kuichukua nafasi hiyo kwenye chati ya nyimbo 100 mashuhuri, ulitolewa. Wimbo wa "Mama Afrika" ulitolewa kama wimbo wa Ulaya mwezi Julai 2007, na kufikisha jumla ya nyimbo nne zilizokuwa zimetolewa kutokwa kwenye albamu hiyo iliyokuwa imefika namba 47 nchini Uingereza.
Kutolewa ya toleo la 'Platinum (Deluxe)' la albamu hii kulifanyika wakati mmoja na kutolewa kwa "Sorry, Blame It on Me", uliokuwa wimbo wa tano kutoka kwa albamu hiyo, na ulioshika nafasi ya saba kwenye orodha ya nyimbo 100 mashuhuri katika mwezi Agosti 2007. Toleo hilo la Deluxe lilitolewa kikamilifu tarehe 28 Agosti 2007. Wimbo wa mwisho katika albamu hiyo ulithibitishwa na Akon kuwa "Never Took the Time." [6] Albamu ya Konvicted ilipata kushika nafasi pili kwenye orodha ya Bango ' la nyimbo 200 mashuhuri, na kuuza nakala 286,000 katika wiki yake ya kwanza. Baada ya wiki sita tu, albamu ya Konvicted iliuza zaidi ya nakala milioni moja nchini Marekani na zaidi ya nakala milioni 1.3 duniani kote. Albamu hii ilithibitishwa kuhitimu kiwango cha platinumu baada ya wiki saba, na baada ya wiki kumi na sita ilithibitishwa kuhitimu kiwango hiki, cha platinamu, kwa mara mbili. Albamu hii ilikaa katika orodha ya nyimbo ishirini za kwanza kwenye orodha ya ' Bango/0} la nyimbo 200 mashuhuri kwa wiki 28 mfululizo na ilipata kushika nafasi ya pili katika nyakati nne tofauti. Mnamo 20 Novemba 2007, shirika la RIAA ilithibitisha albamu hii kuwa imehitimu kiwango cha 'triple platinum' na rekodi milioni 3 zikiwa zimeuzwa Marekani. Imeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani.

Mnamo 5 Oktoba 2006, Akon alivunja rekodi ya orodha ya nyimbo 100 mashuhuri, kwani wimbo wake wa "Smack That" ulipata mafanikio ya juu zaidi kwa kuruka kutoka namba 95 hadi namba 7. Kupanda huko kulitokana na wimbo huo kushika nafasi ya sita kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya Hot Digital Songs kutokana na mipakuo 67000. Rekodi hiyo imevunjwa mara kadhaa tangu wakati huo. Mnamo Desemba 2006, wimbo wa Akon wa "Smack That" ulikuwa umependekezwa kushindana katika kategoria ya Best Rap / Sung Collaboration katika mashindano ya 49 ya Grammy Awards, lakini ulishindwa na ule wa Justin Timberlake na wa T.I. wa "My Love".

Miradi aliyoshirikiana na wasanii wengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Mwaka wa 2006, Akon alianza kampuni yake mpya ya Kon Live Distribution chini ya Interscope Records. Msanii wake wa kwanza kusaini mkataba naye alikuwa ni Ray Lavender.
  • Yeye alishirikishwa kwenye albamu ya hivi karibuni ya Gwen Stefani, The Sweet Escape. Yeye alishiriki katika wimbo wa anwani ya jalada na wimbo wa pili, "The Sweet Escape." Akon alitayarisha wimbo huo. Mnamo 10 Desemba 2006, Akon na Stefani walihudhuria 'Saturday Night Live' kama wageni wanamuziki, hata hivyo hawakuimba wimbo huo kwa sababu Stefani alikuwa bado hajajifunza maneno yake. Hata hivyo, Akon aliimba wimbo huo mbele ya hadhira, katika hafla ya American Idol tarehe 28 Machi 2007 kutokana na Gwen Stefani kushiriki kama kocha usiku uliotangulia. Wimbo huu wa "The Sweet Escape" umefikia # 2 kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri.
  • Akon alishirikiana na Chamillionaire kwenye tepu yake ya, Mixtape Messiah 2, akishiriki kwenye kibao "Ridin 'Overseas" ambacho alikuwa amekitayarisha. Tepu hii ilikuwa tayari kupakuliwa kutoka tovuti ya Chamillionaire kuanzia 24 Desemba 2006.
  • Katika mwaka 2006, baada ya wimbo wao wa mwaka wa 2005 uliotayarishwa na Akon, "Soul Survivor," wawili hawa walisema kuwa kuna mengi zaidi ya kutarajia kutoka kwao katika siku zijazo. Wao walitangaza kuwa kuna mipango ya kushirikiana na kutoa albamu.[7][8]
  • Akon pia alishiriki katika albamu ya Bone Thugs-n-Harmony ya Strength and Loyalty na kwenye albamu ya nane ya Three 6 Mafia, Last 2 Walk, We The Best iliyotayarishwa na DJ Khaled. Aidha yeye alishiriki kwenye albamu ya Fabolous ya, From Nothin' to Somethin ', na wakashiriki wakiwa na 50 Cent katika baadhi nyimbo za Curtis. Isitoshe, yeye alishiriki kwenye [9] albamu ya 5 ya T.I , T.I dhidi ya T.I.P., [10] albamu ya tatu ya Mario Go!, [11] na wakatayarisha wakiwa na Daddy Yankee katika wimbo unaoitwa "Bring It on" kwenye albamu ambayo ilitolewa tarehe 5 Juni 2007.[12]
  • Tarehe 7 Julai 2007 Akon alitumbuiza watu katika hafla ya American leg of Live Earth.
  • Mnamo Novemba 2007, Akon alirekodi toleo jipya la wimbo "Wanna Be Startin 'Somethin'" wakiwa na Michael Jackson. Mwezi wa Februari 2008, toleo jipya la wimbo huo lilitolewa wakati wa maadhimisho ya 25 ya kutolewa upya kwa video ya Michael Jackson ya Thriller. Akon alitayatayarisha kibao cha "Echo" kilicho kwenye albamu mpya ya bendi ya wavulana ya Kilatini, Menudo, kilichotolewa katika majira ya spring ya 2008.
  • Kampuni ya 'Konvict Music' ndiyo ingehusika katika kutolewa upya kwa albamu ya kwanza ya Kat DeLuna, 9 Lives (albamu) ambayo ingeshirikisha Akon katika wimbo wa "Am I Dreaming."
  • Yeye pia alikuwa katika wimbo uliohusisha Aventura, Akon na Wisin Y Yandel ulioitwa "All up 2 you".
  • Katika mwezi wa Julai 2008, wimbo unaoitwa "Hold My Hand" ulisambaa kwenye mtandao. Wimbo huo ni wa R & B ulioimbwa kwa ushirikiano kati ya Michael Jackson na Akon, na uliotungwa na Claude Kelly. Pia kuna toleo lingine la wimbo huo linalomshirikisha Akon pekee. Pia hakuna kutajwa rasmi kwa kurekodiwa kwa wimbo huo katika aidha ya tovuti za wasanii hawa wawili ingawa Akon ameuzungumzia katika tovuti zingine tofauti. Wimbo huu haukujumuishwa katika orodha ya nyimbo za Freedom kama Akon alivyokuwa ameeleza hapo awali. Katika mahojiano na Smiley Tavis, Akon alisema kuwa Jackson alikuwa amepanga kufanya toleo moja la hali ya juu ambalo lingehusisha video ya wimbo huo lakini wimbo huo ulifichuka kwa umma. Huu ndio wimbo wa mwisho unaojulikana wa Jackson kabla ya kifo chake kilichotokea tarehe 25 Juni 2009. Mwishoni mwa Julai ya mwaka huo, wimbo wa heshima ulioandaliwa na Akon unaojulikana kama "Cry Out Of Joy" ilifichuliwa kwenye mtandao.
  • Akon ndiye aliyekuwa pia mtaarishaji mkuu wa albamu ya nne ya Kardinal Offishall, Not 4 Sale, iliyotolewa 9 Septemba 2008. Wimbo wa mauzo wa albamu hiyo, "Graveyard Shift" ulishirikisha Akon, ukiwa pamoja na wimbo wa kwanza, "Dangerous", ambao ulipata kushika nafasi ya # 5 kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri, na ulioshinda tuzo la Wimbo wa Mwaka katika mashindano ya Juno Awards ya 2009.
  • Akon alishiriki katika kuandika na kutayarisha wimbo wa "Put It on My Tab" na New Kids on the Block uliokuwa wa albamu yao ya 2008 Reunion ya The Block.
  • Akon alishiriki katika kuandika na kutayarisha wimbo wa Leona Lewis wa Forgive Me, ulio kwenye albamu yake, Spirit.
  • Kwa sasa yeye anafanya kazi na mshindi wa X Factor 2008, Alexandra Burke kwenye albamu yake ya kwanza.
  • Akon alishiriki katika kutayarisha albamu ya kwanza ya msanii wa Konvict Muzik, Lady Gaga iliyoitwa The Fame na akashiriki katika kuandika & kutayarisha wimbo uliovuma duniani kote wa "Just Dance", ambao pia ulishirikisha Colby O'Donis na uliopendekezwa kushindana katika mashindano ya Grammy Awards ya 51. Wimbo huu uliwapatia vijana hawa wawili wa Konvict Muzik nafasi zao za kwanza za kushindana kwenye mashindano ya Grammy na umefikia namba # 1 katika nchi zaidi ya 14, zikiwa ni pamoja na Australia, Uingereza & Marekani
  • Albamu mpya ya Flo Rida ya R.O.O.T.S. ilishirikisha Akon kwenye wimbo wa "Available".
  • Akon amerekodi wimbo na E-40 unaoitwa "Wake It Up" ulio katika albamu ya E-40 ya The Ball Street Journal. Akon anafanya majaribio na athari za 'auto-tune' katika wimbo huo.
  • Mwimbaji wa Rap, Nelly, alithibitisha kuwa Akon, Pharrell, na T-Pain walizungumza kuhusu kuunda kikundi cha kuimba muziki wa rap katika mwaka wa 2009.[13]
  • Akon pamoja na kampuni yake ya Konvict Muzik pia wanahusika katika kutayarisha albamu ya 2009 ya kikundi cha hip hop / rock, Flipsyde, inayoitwa State of Survival, itakayotolewa kupitia Kon Live Distribution na Cherrytree Records. [14]
  • Akon alifanyakazi na Whitney Houston katika kutayarisha albamu yake mpya ya mwaka wa 2009 iitwayo I Look To You. Yeye alishiriki katika wimbo wa "Like I Never Left".[15]
  • Akon alifanya kazi na kikundi cha bachata kiitwacho Aventura, na waimbaji wa Reggaeton, Wisin y Yandel, katika kutayarisha wimbo wao wa pili wa All Up 2 You kutoka kwa albamu ya Aventura ya The Lastthat iliyotolewa Juni.
  • Akon hivi majuzi alitia saini mkataba na Jayko, msanii wa R & B na Reggaeton kutoka Uhispania, kwenye studio yake na sasa hivi anashirikiana naye kutayarisha albamu yake inayoitwa "Marcando Territorio"
  • Albamu ya Sexy Bitch ilitolewa Julai 2009, kwa ushirikiano na DJ wa Kifaransa, David Guetta.
  • Mnamo Agosti 2009, Akon alitolewa toleo jipya la 'Beautiful' akimshirikisha BOA, mwimbaji maarufu kutoka Korea. Hata hivyo, toleo hili lilikuwa limelenga soko la Ujapani.
  • Akon pia aliimba katika wimbo akishirikiana na Colby O'Donis unaoitwa "What You Got".

Matatizo ya kisheria

[hariri | hariri chanzo]

Mwezi Aprili 2007, Akon alikosolewa baada ya kucheza ngoma ya kusisimua na Danah (Deena) Alleyne, binti wa mhubiri aliyekuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, katika klabu moja huko Trinidad na Tobago, kama sehemu ya shindano bandia, licha ya klabu hiyo kudai kuwa hawaruhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 21, kuingia huko.[16][17] Tukio hilo lilirekodiwa na wafanyakazi wa Akon na baadaye rekodi hiyo ikapakiwa kwenye mtandao. Tarehe 20 Aprili 2007 vyombo vya habari vya mtaa, chaneli TV6, walionyesha video hiyo hadharani. Katikati ukosoaji kwenye redio, televisheni, na kutoka kwa Blogu, Verizon Wireless waliondoa nyimbo za mlio wa simu (ringitoni) zilizoshirikisha nyimbo za Akon. Verizon pia waliamua kutogharamia ziara ya The Sweet EscapeTour ambapo Akon alitarajiwa kuimba mwanzoni mwa onyesho kabla ya Gwen Stefani. kuingia jukwaani [18] Hata hivyo, kampuni ya Universal Music Group haikuchukua hatua dhidi ya Akon, bali iliamrisha tu video hiyo iondolewe kutoka kwa tovuti ya YouTube kutokana na ukiukaji wa hakimiliki. Mtoa maoni na mwanzilishi wa Parents Television council, Brent Bozell aliita hatua hii "ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja." [19]

Wachambuzi wa kisiasa Michelle Malkin, Laura Ingraham, na Bill O'Reilly walimkosoa Akon kwa "kushusha hadhi ya wanawake." [20][21] Malkin alipakia ufafanuzi kuhusu Akon kwenye tovuti ya YouTube, kwa kutumia vijisehemu kutoka kwa video za muziki pamoja na onyesho la Trinidad, na kampuni ya Universal Music Group ikalazimisha kuondolewa kwa video kwa kuwapatia ilani ya kuondoa ya DMCA.[22] Wakfu wa The Electronic Frontier Foundation ilimuunga mkono Malkin katika kupinga kuondolewa huko kwa kusema kuwa hayo ni matumizi mabaya ya hakimiliki, akirejelea matumizi ya haki. [23] Mwezi Mei 2007, UMG walibatiliza madai yao ya video hiyo, na ikarejeshwa kwenye tovuti ya YouTube.

Tarehe 3 Juni 2007, kwenye onyesho la WSPK 's KFEST katika Uwanja wa Dutchess huko Fishkill, New York, mhudhuria mmoja wa onyesho hilo alimtupia Akon kifaa fulani alipokuwa jukwaani. Akon aliuliza umati kumtambua aliyekuwa ametupa kitu hicho na wampeleke jukwaani. Walinda usalama walimshika kijana huyo na kumpeleka hadi jukwaani. Akon kisha alimvuta kutoka kwa umati na kumbeba kwa mabega yake. Kisha akamtupa kijana huyo kwenye umati. Video ya tukio hilo ilitazamwa tena na polisi wa Fishkill.[24] Akon amedai kuwa tukio hilo lilikuwa la maigizo na kwamba yeye alilitumia kuanzisha rekodi yake iliyofuata.[25] Mashtaka ya kuhatarisha ustawi wa kijana, kumdharau, na kumdhulumu, ukiukaji, yaliandikwa, kulingana na ofisa wa polisi Donald F. Williams, na Akon alipelekwa kortini ili kujibu mashtaka haya mawili tarehe 3 Desemba 2007 katika korti la mji wa Fishkill.[26]

2008-hadi leo: Albamu ya Freedom

[hariri | hariri chanzo]

Akon alitoa albamu yake mpya Freedom mnamo 2 Desemba, ambayo imetoa nyimbo nne: "Right Now (Na Na Na)", "I'm So Paid" (akishirikiana na Lil Wayne na Young Jeezy), "Beautiful" (akimshirikisha Kardinal Offishall na Colby O'Donis) na "We Don't Care", Wimbo wa 'We Don't Care' umeshindwa kupanda juu kwenye chati za nchi nyingi, na kufika tu namba 61 katika UK na namba 91 katika Australia kufikia sasa. Albamu hii imefikia kiwango cha dhahabu kwa kuuza zaidi ya nakala 600,000. [onesha uthibitisho]. Baada ya kifo cha ghafla cha mfalme wa Pop Michael Jackson, ambaye Akon alikuwa akifanya kazi naye katika miaka ya mwisho ya Jackson Akon alitoa wimbo wa kuonyesha heshima unaoitwa "Cry Out Of Joy". Akon & Michael Jackson walikuwa marafiki wa karibu katika wakati huu wa mwisho wa maisha ya Jackon.

Akizungumza kuhusu uhusiano wake na Michael Jackson kwa mwandishi anayesifika wa UK wa R & B, Pete Lewis, aliyeshinda tuzo kwa wimbo 'Blues & Soul' katika Oktoba 2008, Akon alisema: "Mike ni Mfalme wa Pop, na nadhani kuwa ni kutimia kwa ndoto kwa msanii yeyote mkuu / mtunzi / mtayarishaji kuweza kufanya kazi na wale waliobora katika biashara! Unajua, kufanya kazi na mtu kama Mike - ambaye amebuni fursa, akafungua milango kwa watu wengi, na kupata mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki, basi - ni tajriba ambayo imetosha kuipokea kwa mtu ye yote! Yaani, wakati mimi nilisafiri kwa ndege hadi Vegas ili nikutane naye, ilikuwa ni kama tulikuwa tumejuana kwa MIAKA! UKWELI! 'Kwa sababu kimuziki tulikuwa na maoni sawa! Uhusiano wetu ulikuwa wa ajabu! Na, kwa hulka zake, alikuwa ndiye mtu mzuri na mnyenyekevu zaidi niliyewahi kukutana naye milele! Yaani, sisi hata tulienda kutazama filamu pamoja - katika wakati wa mchana! Ambayo ilikuwa ni tajriba spesheli! [27]

David Guetta alishirikiana na Akon katika Sexy Bitch, wimbo wa kwanza wa Akon, na umevuma duniani kote. Wimbo huu ambao umekuwa namba # 1 katika zaidi ya nchi 5, na kushika nafasi ya 12 kwenye chati ya Biango la nyimbo 100 mashuhuri, umeshirikishwa kwenye albamu ya Guetta ya One Love. Na ni wimbo wake wa 19 kuingia kwenye orodha ya nyimbo bora 20 duniani kote.

Albamu ya nne ya Akon, Stadium Music inatarajiwa kutolewa 2010.[28]

Televisheni na filamu

[hariri | hariri chanzo]

Akon amethibitisha kwamba anafanyia kazi mradi wa kuanzisha kipindi maalum kwenye televisheni. Kipindi hicho kitaitwa "My Brother's Keeper" na kitahusisha ndungu wawili wa Akon wanaokaribia kuwa mapacha na ambao watazunguka Atlanta wakijifanya kuwa wao ni yeye wa kuwapumbaza watu. Watajaribu kupata huduma za VIP, wasichana na vitu vya bure. Akon amedai kwamba mara nyingi watu huko Atlanta wamedhani kuwa ndugu zake ni yeye na huu ndio msingi wa kipindi hiki.[25]

Akon ana mipango ya kurekodi filamu nzima yenye jina Illegal Alien. Filamu hii imejikita katika baadhi ya matukio ya maisha yake na mwigizaji Mekhi Phifer atamwigiza yeye. Mbali na hayo, Akon alithibitisha katika mahojiano na tovuti ya Poland ya INTERIA.PL mnamo Agosti 2007, kwamba yeye anarekodi filamu inayoitwa "Cocain Cowboys", ambayo inazungumzia maisha ya Jon Roberts, mkuu wa kateli ya Medellin (walanguzi wa madawa ya kulevya wa Colombia).[29] Yeye pia alishirikishwa kwenye tangazo la kibiashara na la kuimba la Verizon Wireless Snitch wakiwa na Obie Trice katika tukio lililoitwa CSI: Crime Scene Investigation "Poppin' Tags."

Mnamo 30 Novemba 2007, Akon aliingia kwenye nyumba ya Big Brother katika Pinoy Big Brother Celebrity Edition 2 kama mgeni ili washiriki waweza kukutana naye kwa sekunde 100 tu.

Yeye pia alionekana kwenye toleo la tarehe 17 Novemba 2008 la WWE Raw, huku Santino Marella akimtaja katika hotuba yake. Kwa sababu ya athari za Kiitaliano za Santino, yeye alilitamka jina la Akon vibaya, yaani "Akorn".

Mnamo 27 Aprili 2008, Akon alionekana na Colby O'Donis katika Dance on Sunset.

Mnamo Februari 2007, Akon alianzisha aina yake ya mavazi, Konvict Clothing. Mavazi haya yalishirikisha mavazi yanayovaliwa mitaani kama jeans za kitambaa cha denimu, fulana zilizo na kofia, t-shati na kofia. Aliuane ni toleo la juu, ambalo linalenga wanaume na wanawake, na linalojumuisha makoti ya aina ya bleza, jeans za kitambaa cha denimu na vitu vingine. Timothy Hodge alionekana kwenye kipindi cha MTV cha Direct Effect wakiwa na Akon wakiwa wanajaribu kukuza mauzo ya mavazi ya Konvict line.[30]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Trouble (2004)
  • Konvicted (2006)
  • Freedom (2008)
  • Stadium Music (2016)
  • El Negreeto (2019)

Tuzo na Uteuzi

[hariri | hariri chanzo]
Akon awards and nominations
Awards and nominations
Award Wins Nominations
American Music Awards
1 3
Grammy Awards
0 5
MTV Video Music Awards
0 4
Totals
Awards won 1
Nominations 12

Akon alipokea uteuzi mara nne ya kushindana kwenye mashindano ya Grammy ya 2008. Uteuzi huo ulikuwa ni katika kategoria za Best Pop Collaboration with Vocals kwa wimbo "The Sweet Escape" wakishirikiana na Gwen Stefani, Best R & B Performance na waimbaji wawili ama kikundi kwa wimbo "Bartender" wakishirikiana na T-Pain, Best Contemporary R & B Album kwa Konvicted, na Best Rap / Sung Collaboration na "I Wanna Love You" wakishirikiana na Snoop Dogg. Tuzo tu ambalo Akon amepokea ni la Mwimbaji wa Kiume wa Soul / R & B anayependwa zaidi kutoka mashindano ya American Music Awards ya mwaka wa 2007. Ujumla, Akon amepokea tuzo moja kutokana na uteuzi wa mara kumi na mbili.

Shindano la American Music Awards

[hariri | hariri chanzo]

Shindani la American Music Awards ni hafla ya kila mwaka iliyobuniwa na Dick Clark katika mwaka wa 1973. Akon amepokea tuzo moja kutokana na uteuzi mara tatu.[31][32]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo -- 2007 | | rowspan = "3" | Akon | | Favourite Soul / R & B Male Artist | | style="background: #99FF99; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="yes table-yes2"|Ameshinda -- | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- Msanii wa Kiume wa Pop / Rock anayependwa | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated

Shindano la Grammy Awards

[hariri | hariri chanzo]

Tuzo za Grammy Awards hutolewa kila mwaka na National Academy of Recording Arts and Science la Marekani. Akon ameteuliwa kwa mashindano mara matano.[31][33]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo -- 2007 | | "Smack That" (na Eminem) | | Best Rap / Sung Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- 2008 | | "The Sweet Escape" (with Gwen Stefani) | | Best Pop Collaboration with Vocals | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- "Bartender" (with T-Pain) | | Best R & B Performance by a Duo or Group | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- Konvicted | | Best Contemporary R & B Album | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- "I Wanna Love You" (na Snoop Dogg) | | Best Rap / Sung Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated

Tuzo za MTV Video Music Awards

[hariri | hariri chanzo]

Tuzo za MTV Video Music Awards ni hafla ya mwaka iliyoanzishwa mwaka 1984 na MTV. Akon ameteuliwa kwa mashindano mara nne.[31][34][35]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo -- 2005 | | "Locked Up" | | MTV2 Award | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- 2007 | | Akon | | Male Artist of the Year | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- | Most Earthshattering Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated -- | Most Earthshattering Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated
  1. "Akon apologizes for sexually explicit dance", CNN, 2007-05-10.
  2. "Akon Apologizes For Racy Onstage Dance Ilihifadhiwa 18 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.", Billboard, 2007-05-09.
  3. Akon at The Ellen Degeneres Show and in other interviews (7 Januari 2009).
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-16. Iliwekwa mnamo 2009-11-30.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-15. Iliwekwa mnamo 2009-11-30.
  6. Tang, Melisa. Akon: The Good The Bad, Ilihifadhiwa 7 Februari 2009 kwenye Wayback Machine. BallerStatus.com, 2007/08/02.
  7. Reid, Shaheem. Saga Of Young Jeezy, Akon Continues With Possible Duet LP, Ilihifadhiwa 9 Januari 2010 kwenye Wayback Machine. MTV News, 2006/06/15.
  8. Petipas, Jolene. Young Jeezy Teams With Akon For Collabo CD, Ilihifadhiwa 27 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. SOHH, 2006/12/07.
  9. "My List: Akon". Ilihifadhiwa 16 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine. Rolling Stone, 2007/04/03.
  10. Kohen, Jonathan. "TI Stretches Out With Eminem, Timbaland, Wyclef", Ilihifadhiwa 18 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. Billboard, 2007/04/14.
  11. Rodriguez, Jayson. "Mario Gets Back To Making Music With Akon, Timberland, Neptunes", Ilihifadhiwa 29 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine. MTV.com, 2007/04/13.
  12. Cohen, Jonathan. "Daddy Yankee Drafts Fergie, Akon For New Album", Ilihifadhiwa 26 Julai 2008 kwenye Wayback Machine. Billboard, 2007/04/03.
  13. Goldstein, Melissa (2008-10-23). "Pharrell, T-Pain, Nelly, Akon Unite for Supergroup". Spin. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-29. Iliwekwa mnamo 2009-11-30.
  14. . /flipsyde "Flipsyde's Official MySpace". {{cite web}}: Check |url= value (help)
  15. "MTV: Whitney & akon Collab". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-22. Iliwekwa mnamo 2009-11-30.
  16. Telesford, Nigel. Akon 'Africa' Trinidad, Ilihifadhiwa 14 Mei 2007 kwenye Wayback Machine. Trinidad Express, 2007/04/14.
  17. Ramnarine, Kristy. Zen mmiliki: for club, Ilihifadhiwa 1 Julai 2007 kwenye Wayback Machine. Trinidad Express, 2007/04/20.
  18. Leeds, Jeff. Verizon Drops Pop Singer From Ads, New York Times, 2007/05/10.
  19. Bozell, L. Brent III. Rapper Not a "Perfect Gentleman", Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. ParentsTV.org, 2007/05/24.
  20. Malkin, Michelle. Look who's Promoting a vulgar misogynist, MichelleMalkin.com, 2007/05/03.
  21. Pulse Report, Ilihifadhiwa 11 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. SOHH.com, 2007/05/11.
  22. Malkin, Michelle. "Akon's record company abuses DMCA kwa Rose to stifle criticism on YouTube", MichelleMalkin.com, 2007/05/03.
  23. "Malkin Fights Back Against Copyright Law Misuse by Universal Music Group", Electronic Frontier Foundation, 2007/05/09.
  24. Police: Akon investigation continues, Ilihifadhiwa 16 Januari 2016 kwenye Wayback Machine. Poughkeepsie Journal, 2007/08/29.
  25. 25.0 25.1 Sawjani, Archna. Akon: Real Talk, Ilihifadhiwa 20 Julai 2008 kwenye Wayback Machine. AllHipHop.com, 2007/08/06.
  26. Akon Faces Charges, Poughkeepsie Journal, 2007/11/30.
  27. "Akon interviewed by Pete Lewis, 'Blues & Soul' December 2008". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-10. Iliwekwa mnamo 2009-11-30.
  28. Akon Preps New Album. Vibe.
  29. "Akon intensywnie", Archived 2012-07-12 at Archive.today INTERIA.PL, 2007/08/28.
  30. Winning, Brolin. "Akon - Got It Locked Ilihifadhiwa 4 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. ", MP3.com, 2006/10/23.
  31. 31.0 31.1 31.2 "Akon". Rock on the Net. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
  32. Cohen, Sandy (2007-11-19). "Daughtry Wins 3 American Music Awards". The Washington Post. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
  33. Montgomery, James (2007-12-06). "Akon Calls His Mom, Plain White T's Call Delilah To Celebrate Grammy Nominations". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-06. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
  34. "2005 Video Music Awards". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-28. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
  35. "2007 Video Music Awards". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-17. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: