Wazazi wake wote wanatokea huko Dominika, mama yake, ana miliki duka la mikate mjini mwa mji wa Newark. Kwa sasa ameingia mkataba na studio ya Epic Records/GMB na studio ya Akon maarufu kama Konvict Muzik.
Konvict imetoa kile cha moyoni kwa kusema kuwa wanampango wa kuitoa upya albamu yake ya kwanza ya mwanadada huyu ya 9 Lives, lakini maelezo yake wa hivi karibuni alioyatoa kupitia mtandao wa myspace na kusema kwamba, amerejea zake studio kwa ajili ya kutoa albamu ya pili, na kupendekeza kuwa albamu ya 9 Lives haito tolewa tena, bali atashughulikia albamu mpya tu.