Nenda kwa yaliyomo

Justin Timberlake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Justin Timberlake
Justin Timberlake.
Justin Timberlake.
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Justin Timberlake
Nchi Marekani
Alizaliwa 31 Januari 1981
Aina ya muziki Pop na R&B
Kazi yake Mwanamuziki
Mwigizaji

Justin Timberlake (amezaliwa Memphis, Tennessee, 31 Januari 1981) ni mwimbaji wa muziki wa pop na R&B kutoka nchini Marekani.

Timberlake alianza kujipatia umaarufu kwa kucheza kipindi cha televisheni Mickey Mouse Club kilichokuwa maalum kwa ajili ya watoto. Baadaye akawa mmoja wa washindi wa tuzo ya Grammy-bendi bora ya vijana *NSYNC. Baadaye TENA alianza kuimba kama msanii pekee akafanikiwa kutoa albamu mbili za muziki, Justified na FutureSex/LoveSounds.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Kwa asili ukoo wa Timberlake ulitokea Uingereza, na familia walikulia katika imani za Kibaptisti. Wazazi wake walitengana mnamo mwaka wa 1985 na baada ya hapo, mama yake aliolewa tena, na vilevile baba akaoa mke mwingine. Maisha yake yote alikulia Millington, Tennessee, mji mdogo kaskazini mwa Memphis.

Mnamo mwaka 1993, Timberlake akajiunga na Mickey Mouse Club, mfululizo wa kipindi cha televisheni kilichoshirikisha wasanii walio wengi vijana. Hiyo ndiyo ikawa mara yake ya kwanza kuonja ladha ya umashuhuri. Na katika kipindi hicho Timberlake alishiriki kuanzia msimu wa sita na saba tu.

Wakati wa maonyesho ya kipindi hicho, Timberlake akakutana na aliyewahi kuwa mpenzi wake (Britney Spears), na wengine alikuwemo Christina Aguilera, na mshirika mwenzake wa katika bendi bwana JC Chasez. Ilivyofika mwaka 1995 kipindi kiliisha, na Timberlake akajiunga na bwana Chasez na washikaji wengine, wakaanzisha kundi la muziki lilojulikana kwa jina la *NSYNC".

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Timberlake alianza mambo ya mapenzi akiwa yungali mdogo sana, wa kwanza kuwa naye alikuwa mwanafunzi mwenziye na baada ya hapo mwanamuziki wa pop, Veronica Finn, lakini penzi lao halikudumu sana, wakaachana pasipo na amani.

Baadaye alianza uhusiano na mwanamuziki Britney Spears, mara tu walipokutana katika kipindi cha televisheni cha Mickey Mouse Club. Mahusiano hayo yalikuwa gumzo kubwa kwa jamii yakaisha ghafla mwaka 2002 baada ya Timberlake kumshutumu Spears kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwalimu wa ufundishaji muziki wa ku-densi, Wade Robson.

Mwaka wa 2002, akawa na mahusiano ya kimapenzi na mchezaji wa muziki-mwigizaji Jenna Dewan, vilevile na mwigizaji-mwimbaji Alyssa Milano. Mnamo Aprili 2003, akaanza mahusiano na mwigizaji wa filamu Cameron Diaz baada ya kukutana katika sherehe za ugawaji wa tuzo za vijana za Nickelodeon Kids' Choice.

Baada ya hapo kukawa na fununu nyingi tu zenye kuelezea kwamba wapenzi hao washaachana, lakini tarehe 16 Desemba 2006 mnamo siku ya Jumamosi katika kipindi cha televisheni kilichokuwa kinarushwa hewani moja kwa moja nyakati za usiku, Timberlake alithibitisha kwamba wawili hao ni kweli hawana mahusiano tena.

Mnamo mwaka 2007, ilijulikana kwamba Tilmberlake ana mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji wa filamu Jessica Biel.

Nyimbo na albamu[hariri | hariri chanzo]

Albamu alizotoa[hariri | hariri chanzo]

 • 2002 - Justified
 • 2006 - FutureSex/LoveSounds
 • 2013 - The 20/20 Experience
 • 2013 - The 20/20 Experience – 2 of 2
 • 2018 - Man of the Woods
 • 2024 - Everything I Thought It Was

Nyimbo maarufu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Nyimbo Albamu
2002
 • "Like I Love You"
 • "Cry Me a River"
 • "Rock Your Body"
 • "Señorita"
Justified
2006
 • "SexyBack" akishirkiana na Timbaland
 • "My Love" akishirkiana na T.I.
 • "What Goes Around...Comes Around"
 • "Summer Love"
 • "LoveStoned"
 • "Until the End of Time"
FutureSex/LoveSounds

Nyimbo alizoshirikishwa[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo maarufu za Justin Timberlake ambazo alirekodi na wanamuziki wengine:

Filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]

 • Model Behavior (2000)
 • Edison Force (2005)
 • Alpha Dog (2006)
 • Black Snake Moan (2007)
 • Shrek the Third (2007)
 • Southland Tales (2008)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. http://www.imdb.com/name/nm0005493/
 2. http://www.gm.tv/index.cfm?articleid=21993 Archived 27 Machi 2008 at the Wayback Machine.
 3. Teaching That Makes a Difference: How to Teach for Holistic Impact

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]