Britney Spears
Britney Spears | |
---|---|
Spears, Mei 2013
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Britney Jean Spears |
Amezaliwa | 2 Desemba 1981 McComb, Mississippi, United States |
Asili yake | Kentwood, Louisiana, United States |
Aina ya muziki | Pop, dance, R&B |
Kazi yake | Mwimbaji, dansa, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji, mtunzi wa nyimbo, mpiga piano, mwongozaji |
Ala | sauti, piano |
Aina ya sauti | Soubrette[1] |
Miaka ya kazi | 1993–mpaka sasa |
Studio | Jive |
Ame/Wameshirikiana na | The New Mickey Mouse Club, Innosense |
Tovuti | www.britneyspears.com www.britney.com |
Britney Jean Spears (alizaliwa tar. 2 Desemba 1981 mjini Kentwood, Louisiana) ni mwanamuziki wa Pop na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani.
Mafanikio ya awali
[hariri | hariri chanzo]Britney Spears alikuwa akiigiza katika kipindi cha TV cha watoto kilichokuwa kinarushwa hewani kati ya 1991 na 1995. Kipindi kilijulikana kwa jina la New Mickey Mouse Club na kilikuwa kinatayarishwa na kampuni ya Walt Disney Productions. Watu wengine waliokuwemo na kushiriki katika kipindi hicho, alikuwa Christina Aguilera, Justin Timberlake, na JC Chasez (ambaye baadaye alikuja kuwa mmoja wa wanabendi ya *NSYNC), na waigizaji Ryan Gosling na Keri Russell.
Mnamo mwaka wa 1998, Britney alitoa kibao chake cha kwanza kilichokwenda kwa jina la "...Baby One More Time". Video ya nyimbo hiyo ya Baby One More Time imekuwa maarufu sana kutokana inaonyesha Britney amevaa sare za wanafunzi wa shule ya Wakatoliki.
Albamu alizotoa
[hariri | hariri chanzo]Britney ametoa albamu 8. Albamu hizo ni kama ifuatavyo:
- ...Baby One More Time (1999)
- Oops!... I Did It Again (2000)
- Britney (2001)
- In The Zone (2003)
- Greatest Hits: My Prerogative (2004)
- B In The Mix: The Remixes (2005).
- Blackout (2007).
- Circus (2009)
- Femme Fatale (2011)
- Britney Jean (2013)
Filamu alizoiigiza
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2002, Spears amecheza filamu ya Crossroads.
Mwaka huo huo wa 2002, Britney amecheza tena filamu ya Austin Powers in Goldmember.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tar. 3 Januari ya mwaka wa 2004, Spears akaolewa na kijana waliokuwa ote toka utoto Nd. Jason Allan Alexander, mjini Las Vegas, Nevada, Marekani. Ndoa haikudumu sana na baadaye wakatarikiana.
Mnamo mwezi wa Septemba ya tarehe 18 katika mwaka 2004, Spears akaolewa tena na bwana Kevin Federline. Kwa pamoja wakabahatika kupata mtoto wa kiume aliojulikana kwa jina la Sean Preston Spears Federline, aliz. tar. 14 Septemba 2005. Kunako 12 Septemba mwaka 2006, Britney akajaaliwa kupata mtoto mwigine wa kiume aliyejulikana kwa jina la Jayden James Spears Federline.
Kunako mwezi wa Novemba 2006, Spears akafungua jalada la kudai taraka kutoka kwa mumewe bwana Kevin.
Mnamo mwezi Septemba ya mwaka wa 2007, Spears amepoteza haki ya kuwa na watoto wake wawili aliyezaa na bwana Kevin Federline, watoto hao ni Sean Preston na Jayden James.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Tovuti zake zilizo rasmi
[hariri | hariri chanzo]Tovuti za mashabiki wa Britney
[hariri | hariri chanzo]- UKBritney
- Fansite (2) Archived 23 Desemba 2007 at the Wayback Machine.