The Fame ni jina la kutaja albamu ya kwanza ya mwanamuziki wa pop dansi wa Kimarekani Bi. Lady Gaga. Albamu ilitolewa mnamo mwezi wa Agosti katika mwaka wa 2008 - na ilitolewa chini ya Interscope Records kwa Kanada na baadhi ya nchi za Ulaya. Toleo la pili la albamu hiyohiyo iliyokuwa na baadhi ya nyimbo tofauti kadhaa na ilitolewa kunako tar. 15 Novemba 2008 kwa ajili ya Australia tu. Kunako tar. 28 Oktoba ya mwaka wa 2008, albamu ilitolewa kwa nchi ya Marekani. Kunako tar. 9 Januari ya mwaka wa 2009, albamu ilitolewa kwa ajili ya nchi ya Ireland na UK, hadi kufikia 12 Januari 2009.
Albamu ilifikia katika chati za Billboard Electronic Albums na vilevile kushika cha za Kanada na Ireland pia. Single mbili za mwanzo kutoka katika albamu hiyo ni pamoja na "Just Dance" na Poker Face", zimepata mafanikio makubwa makubwa dunia nzima na pia kushika chati kibao za Marekani na Uingereza pia.