Mkoa wa Simiyu
Mandhari
Mkoa wa Simiyu ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 39000 [1]. Ulianzishwa rasmi Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Shinyanga upande wa mashariki[2].
Makao makuu yako Bariadi.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Kadiri ya sensa ya mwaka 2022, mkoa una wakazi 2,140,497 [3] kutoka 1,584,157 wa mwaka 2012, [4] walipokuwa wameongezeka 1.8% kwa mwaka katika miaka 2002-2012[4].
Msongamano wa watu ulikuwa 63 kwa kilometa mraba.[4]
Kabila kubwa ni lile la Wasukuma.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Mkoa huo mpya una wilaya 6 zifuatazo: Bariadi Mjini, Bariadi, Busega, Maswa, Meatu, Itilima.
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Bariadi : mbunge ni Andrew Chenge (CCM)
- Busega : mbunge ni Raphael Chegeni (CCM)
- Itilima : mbunge ni Njalu Silanga (CCM)
- Kisesa : mbunge ni Luhaga Mpina (CCM)
- Maswa Mashariki : mbunge ni Stanslaus Nyongo (CCM)
- Maswa Magharibi : mbunge ni Mashimba Ndaki (CCM)
- Meatu : mbunge ni Salum Khamis Salum (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Staff. "Tanzania: State Gazettes New Regions, Districts", 9 March 2012. Retrieved on 2017-08-22. Archived from the original on 2012-08-23.
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ 4.0 4.1 4.2 "Population Distribution by Administrative Units, United Republic of Tanzania, 2013" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-05-02. Iliwekwa mnamo 2017-08-22.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Serikali ya Tanzania
- Wasukuma Ilihifadhiwa 3 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |