Wasukuma
Wasukuma ni kabila kubwa kutoka eneo la kusini na mashariki mwa Ziwa Viktoria, nchini Tanzania. Kabila hili hasa huishi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Mwaka 2002 idadi ya Wasukuma ilikadiriwa kuwa 3,200,000 [1]. Lugha yao ni Kisukuma. Kisukuma ni miongoni mwa lugha za Kibantu ambazo hubainishwa kama lugha mabishi.
[hariri] Shughuli za kiuchumi.
Shughuli kuu za kiuchumi kwa wasukuma ni kilimo,uvuvi, ufugaji na biashara. Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku, mahindi,Viazi,Dengu na matunda(Kisiwani ukerewe) Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo huchimbwa katika maeneo mbali mbali mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Wasukuma pia wanajihusisha sana sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbali mbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama Mahindi na Mpunga.
[hariri] Maeneo yaliyo na madini
Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali. Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini.
1.Mwadui (Huku kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia serikali pesa za kigeni) 2. Maganzo (Vilevile eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui.)
| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasukuma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Makala hiyo kuhusu "Wasukuma" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema. |