Malaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbu wa Anopheles akishiba damu na labda kumwambukiza mtu

Malaria ni ugonjwa unaoleta homa kali na kusababishwa na kimelea yaani kidudu kidogo katika damu. Malaria huambukizwa kwa njia ya kudungwa na mbu mwenye vilemea hivi ndani yake.

Kimelea kinachosababisha malaria huitwa plasimodi (plasmodium) ni kiumbe kidogo chenye seli moja tu. Huzaa ndani ya mbu aina ya Anopheles halafu inahitaji kuhamia katika damu ya mwanadamu na hapa zinasababisha vurugo kwa kuharibu seli nyekundu za damu na kusababisha homa. Kama mtu mgonjwa anadungwa na mbu asiye na kimelea hiki uogonjwa unaingia katika mbu aliye tayari kuwaambukiza watu tena.

Kuna aina mbalimbali ya plasimodi zinazosababisha aina tofauti za malaria zinazotibiwa kwa madawa mbalimbali.

  • Plasmodium falciparum
  • Plasmodium knowesli
  • Plasmodium malariae
  • Plasmodium ovale
  • Plasmodium semiovale
  • Plasmodium vivax

P. vivax na P. falciparum zinasababisha malaria kwa watu wengi. Falciparum ni mbaya zaidi na kuua watu wengi kushinda aina nyingine.

Plasimodi jinsi inayoonekana kwa hadubini

Yaliyomo

[hariri] Hatari za malaria

Kila mwaka watu milioni 300 - 700 huambukizwa malaria. Watu milioni 1 - 2 hufa kila mwaka na walio wengi wako Afrika. Asilimia 20 za watoto wa Afrika wanaofariki chini ya umri wa miaka 5 hufa kwa sababu ya malaria. Wengine hubaki na athira mbaya kwa afya yao hata kwa ubongo.

Malaria husababisha homa inayoendelea kuwa kali. Homa kali sana juu ya sentigredi 41 inaweza kuua watu. Malaria inayoendelea kwa muda inaharibu seli nyekundu za damu. Inaweza kuharibu pia mafigo.


[hariri] Kuambukizwa

Mtu humabukizwa kwa kudungwa na mbu wa Anopheles mwenye vilemea hivi ndani yake. Plasimodi inaingia ndani ya damu wakati mbu inamdunga mtu kwa sababu imo ndani ya mate ya mbu. Mate ya mbu huingia ndani ya damu ikibeba kimelea cha plasimodi ndani yake. Baada ya muda wa wiki moja hadi nne ugonjwa unaanza kwa homa.

Kati ya mbu za Anopheles ni jike tu zinazobeba plasimodi kwa hiyo ni jike tu zinazoweza kuambukiza watu. Hawapendi kuruka wakati wa jua kali lakini jioni na usiku wako kazini.

[hariri] Kumabukizwa kutegemeana na wakati na tabianchi

Kidudu cha plasmodi inahitaji halijoto ya angalau sentigredi 15-16 kwa kuiva ndani ya mbu. Kwa sababu hii haiwezi kuzaa wakati halijoto inashuka chini ya kiwango hiki. Lakini katika nyanda za chini penye halijoto mwaka wote malaria inaendelea mfululizo.

Hapa ni sababu ya kwamba hakuna malaria ya kudumu katika nyanda za juu za Afrika ya Mashariki ambako halijoto inashuka wakati wa usiku kwa miezi kadhaa.

[hariri] Mfano wa Nairobi

Nairobi kwa mfano haina malaria ya kudumu yaani watu hawaambukizwi pale mwaka wote. Kwa bahati mbaya maisha ya kisasa imeongeza usafiri unaosafirisha pia mbu pamoja na malaria ndani yake. Kama mbu mwenye plasimodi ndani yake inafika katika ya mzigo wa ndizi kutoka nyanda za chini inabeba ugonjwa ndani yake inaweza kuwambukiza watu.

Kama ambukizo hili linatokea wakati wa baridi mtu huyu huwa mgonjwa lakini ugonjwa hauendelei. Ila tu kama ambukizo linatokea wakati wa joto hata hewa ya Nairobi iko juu ya sentigredi 16 na ugonjwa utaendelea. Mtu anaambukizwa; ugonjwa unaendelea ndani yake akidungwa na mbu safi hata mbu hii anashika malaria na kuwaambukiza watu wengine. Sasa hatari ya kuambukizwa inategemea mahali ndani ya Nairobi. Watu wanaoishi katika mitaa ya vibanda tena karibu na masoko hukaa hatarini kuliko watu wanaoishi katika mitaa kama Runda. Katika mitaa ya vibanda huwa na matopematope na mahali ambako mbu huzaa. Mitaa ambayo ni mbali na barabara na masoko ni bora kwa afya kwa sababu mbu huishi muda mfupi tu na hazitembei mbali sana.

Lakini mtu anayebeba plasmodi ndani yake anaweza kufika kila mahali na kudungwa na mbu safi anayeambukizwa kwa njia hiyo na kama ni kipindi cha joto malaria inaweza kuendelezwa kila sehemu.

Nchi penye Malaria duniani

[hariri] Uenezaji wa Malaria

Kwa jumla Malaria imeenea katika nchi zote za joto. Katika maeneo makavu pasipo na nafasi nzuri kwa mbu iko kidogo tu au imepotea.

Kuna hatari ya uenezaji wa Malaria. Nchi kama Marekani, Italia na Ujerumani zilikuwa na kiwango fulani cha Malaria wakati wa joto. Walifaulu kumaliza mbu wote wenye plasimodi lakini Anopheles bado iko. Kama halijoto ya dunia inapanda na wasafiri kutoka nchi za kusini wanaingiza malaria kuna hatari ya kurudi kwa ambukizo la malaria katika nchi hizi za kaskazini.

Tayari sasa kuna maambukizo machache yanayoitwa "malaria ya uwanja wa ndege" yanatokea kama mbu mwenye plasimodi aliyebebwa ndani ya mzigo wa ndege anafika huko wakati wa joto na kudunga watu. Hutokea karibu na uwanja wa ndge tu.

[hariri] Kupambana na malaria

Njia bora ni kuzuia malaria badala ya kumabukizwa na kuitiba.

Malaria inazuiliwa kwanza kwa kuzuia kudungwa. Njia yake ni:

  1. kutumia nyavu ya mbu wakati wa kulala
  2. kuzuiya mbu ndani ya nyumba kwa nyavu madirishani
  3. kuvaa nguo ndefu nje ya nyumba wakati wa giza na kutumia madawa ya kupakaa usoni, mkononi na mguuni
  4. kupuliza dawa la kuua mbu ndani ya nyumba
  5. kutoacha akiba ya maji karibu na nyumba (bwawa, pipa, matope) kwa sababu bila maji mbu hawezi kuzaa na hatembei mbali sana.
  6. kupanda miti ya mwarobaini karibu na nyumba kwa sababu mbu hapendi harufu

Baada ya kuambukizwa kuna madawa mbalimbali lakini ni muhimu kupata ushauri wa daktari kwa sababu si kila homa ambayo ni malaria. Tena kuna aina tofauti za malaria zinazohitaji madawa tofauti.

[hariri] Viungo vya Nje