Kuku
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kuku | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kuku: Jogoo na tembe
|
||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Kuku ni ndege anayefugwa na binadamu tangu miaka 8,000. Watu hutumia nyama yake na mayai kama chakula. Katika nchi ya baridi malaika yao ambayo ni manyoya madogo ya chini yanatumiwa kwa kujaza mashuka au makoti. Samadi ya kuku ni mbolea mzuri lakini inapaswa kukaa kwa muda kabla ya kutumiwa.
Kuku dume huitwa jogoo na jike ni tembe; mtoto wa kuku ni kifaranga. Kutokana na ufugaji uwezo wa kuruka umepotea.
Idadi ya kuku duniani inakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 10 na wengi wanafugwa kwa wingi wakiotomiwa na kuishi zizini. Kwa njia ya ufugaji aina nyingi za kuku zimeendelezwa kwa kuchagua wanyama wenye tabia maalumu na kuwazaaliana. Wanaofugwa siki hizi ni aina zinazotoa hasa nyama na aina nyingine zinatoa hasa mayai.
Katika mazingira asilia kuku huishi miaka 5-11 lakini wale wanaofugwa kwa wingi wanachinjwa baada ya wiki 6-8 kama ni kuku wa nyama na mwaka mmoja kama ni kuku wa mayai. Kati ya aina zinazofugwa kwa mayai karibu dume wote yaani nusu ya vifaranga wanauawa mara moja kwa sababu hawategi mayai na aina hii haileti nyama ya kutosha.
Asili ya kuku zetu ni kuku mwitu wa Indonesia. Ufugaji wake ulisambazwa Asia Bara na Polynesia. Mabaki ya mifupa ya kuku yamepatikana China ykiwa na umri wa miaka 8,000. Kutoka Asia ya Kusini-Magharibi kuku walisambazwa Uhindi na kupita Uajemi hadi Ugiriki na Ulaya. Inaaminiwa ya kwamba kuku walifika Amerika Kusini kabla ya kuja kwa Kolumbus kupitia Pasifiki.
[hariri] Picha
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kuku kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |