Zheng He

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha:Zheng He.jpg
Picha ya kisasa ya Zheng He

Zheng He (1371-1433) alikuwa baharia, kiongozi wa kijeshi na mpelelezi kutoka China wakati wa nasaba ya Ming. Aliongoza misafara ya jahazi zake hadi pwani za Afrika hadi Msumbiji akapeleleza Bahari Hindi na visiwa vya Asia ya Kusini-Mashariki.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Zheng He alizaliwa katika familia ya Wachina Wasislamu kwenye jimbo la Yunnan kwa jina la Ma He. Baba yake aliwahahi kusafiri Maka kwa hajj. Katika vita kijana alikamatwa kama mfungwa akafikishwa kwneye makao makuu ya Kaisari wa China. Hapa alihasiwa kuwa towashi jinsi ilivyokuwa kwa watumishi wa wafalme huko China.

Alikuwa rafiki wa mtoto wa Kaisari akafundishwa pamoja naye katika mengi. Huyu alipokuwa Kaisari mwenyewe kwa jina la Yongle alimpa madaraka juu ya jeshi la bahari.

Twiga kutoka Malindi ilifika China kwa meli za Zheng He

Safari[hariri | hariri chanzo]

Kati 1405 na 1433 Zheng He aliongoza misafara 7 za baharini kama kiongozi wa vikundi vikubwa vya meli. Meli zake zilikuwa jahazi kubwa sana zilizobeba hadi tani 1500. Kila safari Zhenh He alipewa meli 50-60 na idadi ya wanajeshi na mabaharia ilikuwa takriban 25,000 - 30,000.

Meli za Zheng He kwenye picha ya Kichina ya karne ya 16

Safari tatu za kwanza zilipeleleza maeneo yanayoitwa leo Indonesia, Uhindi na Sri Lanka. Katika safari za tatu hadi saba aliendelea hadi pwani za Afrika.

1413–1415 alisafiri mara ya kwanza Afrika ya Mashariki. Alitembelea Mogadishu na Malindi kwenye pwani la Kenya. Sultani wa Malindi alimtuma balozi na meli za Zheng He aliyeleta twiga kama zawadi kwa Kaisari wa China. Mnyama huyu alisababisha Wachina kushangaa na kuna picha yeke iliyochorwa wakati ule.

Kufika hadi Atlantiki na Amerika?[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu kadhaa wamedai ya kwamba kwenye safari ya 1521 kundi dogo la meli zake liliingia Atlantiki na kuivuka hadi kufika Amerika. Lakini hii inapingwa na wataalamu wengi.

Hata hivyo kuna ramani ya dunia ya Mwitalia Fra Mauro ya mwaka 1459 aliyechora meli ya Kichina katika Atlantiki pamoja na maelezo ya kwamba yeye alipata habari kuhusu meli kubwa kutoka mashariki iliyoingia Atlantiki. Maelezo yale hayaeleweki kabisa kwa sababu wakati ule Wareno hawakufika bado kusini ya Afrika wala hawakuingia Bahari Hindi bado na Amerika haikujulikana hivyo Fra Mauro hakuwa na majina kwa yale aliyosikia.

Zheng alikufa ama wakati wa safari yake ya mwisho au mara moja baada ya kurudi akazikwa karibu na mji wa Nanjing.

Mwisho wa safari[hariri | hariri chanzo]

Makaisari wa baadaye walisimamisha safari. Mtindo wa Zheng He ulikuwa na gharama kubwa sana. Yote ililipiwa na sertikali kuu na gharma zilipita faida ya bidhaa zilizoletwa. Tofauti na safari za Wareno na Wahispania za baadaye Wachina hawakulenga faida ya kibiashara.

Meli zilifungwa bandarini zikaoza polepole.