Yohane Ogilvie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. John Ogilvie
Kifodini cha Mt. John Ogilvie.

John Ogilvie (Drumnakeith, Banffshire, 1579Glasgow Cross, 10 Machi 1615) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uskoti.

Mtoto wa kwanza wa Walter Ogilvie, Mkalvini tajiri, alipokuwa na umri wa miaka 12 alitumwa Ulaya bara kwa masomo.

Mwaka 1596 alijiunga na Kanisa Katoliki huko Leuven, Ubelgiji, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Yesu.

Alipata upadrisho huko Paris, Ufaransa, mwaka 1610. Akifanya uchungaji huko Rouen, Normandy, aliomba mara kadhaa kutumwa Glasgow (ingawa tangu mwaka 1560 huko Uskoti ilikuwa marufuku kutetea Ukatoliki).[1]

Alipokosa msaada huko, alikwenda London, Uingereza, tena Paris, na mnamo Novemba 1613 akarudi Uskoti akijidai ni mfanyabiashara, jina lake John Watson. Kumbe alianza kuhubiri na kusoma Misa kwa siri hadi Oktoba 1614, alipofungwa gerezani.

Hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande.[2]

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976.[3]

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 10 Machi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Patron Saints Index: Saint John Ogilvie (2009-01-15). Jalada kutoka ya awali juu ya 15 January 2009.
  2. 10. mars: Den hellige John Ogilvie (~1580-1615) (2010-03-13). Jalada kutoka ya awali juu ya 13 March 2010.
  3. Irondequoit Catholic Communities - - John Ogilvie (2008-10-11). Jalada kutoka ya awali juu ya 11 October 2008.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yohane Ogilvie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.