Yohane Mwenyehuruma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yohane Mwenyehuruma katika kanisa lake huko Venezia, Italia.

Yohane Mwenyehuruma (Amathus, Kupro, 550 - Amathus, 616) alikuwa Patriarki wa Aleksandria, Misri.

Aliitwa Mwenyehuruma kutokana na ukarimu wake mkubwa kwa fukara[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[2] au kesho yake.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa gavana wa Kupro, alioa na kupata mwana mmoja, lakini baada ya muda mfupi alifiwa mke na mtoto alishika maisha ya utawa.

Mwaka 608 akawa Patriarki akasaidia wakimbizi kutoka Nchi Takatifu walioshambuliwa na Waajemi, lakini hatimaye kwa vitisho vyao alirudi Kupro.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.