Yohane Climacus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya karne ya 13 ikimuonyesha Yohane Climacus; kandokando kuna Mt. George na Mt. Blaise (Shule ya Novgorod, Urusi).

Yohane Climacus (kwa Kigiriki Ἰωάννης τῆς Κλίμακος, yaani Yohane wa Ngazi; 525 - 606) alikuwa mmonaki katika monasteri ya Mlima Sinai.[1] Ni maarufu kwa maandishi na miujiza yake.

Toka zamani anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Machi[2].

Kitabu cha Ngazi[hariri | hariri chanzo]

Habari za maisha yake ni chache, lakini tuna kitabu chake Κλῖμαξ (Ngazi)[3] na kingine kifupi zaidi Kwa Mchungaji ambacho ni kama nyongeza yake.[4]

Picha takatifu ya Ngazi, ikimuonyesha Yohane Climacus akiongoza wamonaki wanaopanda ngazi, iliyochorwa katika karne ya 12 (iko Monasteri ya Mt. Katerina, Mlima Sinai, Misri).

Humo Yohane anasimulia namna ya kuinua roho na mwili wetu kwa Mungu kwa kujipatia maadili, akitumia ndoto ya ngazi aliyoiona Yakobo-Israeli kama fremu ya kutolea mafundisho yake ya kiroho.

Kila sura inahusu "kidato" kimoja, yaani mada moja. Jumla ya vidato vyote vya ngazi ni 30. Saba vya kwanza vinahusu maadili ya msingi kwa maisha ya juhudi. Vile 19 vinavyofuata (8–26) vinahusu ushindi juu ya vilema na upatikanaji wa maadili yaliyo kinyume chake. Vile 4 vya mwisho vinahusu maadili makuu yaliyo lengo la juhudi zote, hasa upendo (ἀγάπη).

Ingawa walengwa asili wa kitabu walikuwa wamonaki wa monasteri ya jirani, mapema Ngazi kikawa kati ya vitabu vilivyopendwa zaidi katika Ukristo wa mashariki, na kinasomwa sana, hata katika liturujia, hasa wakati wa Kwaresima Kuu kabla ya Pasaka.

Picha ya Ngazi[hariri | hariri chanzo]

Picha takatifu yenye jina hilohilo, Ngazi ya Kupanda kwa Mungu, inaonyesha ngazi ambayo kutoka duniani inafika mbinguni (taz Mwa 28:12). Wamonaki wengi wanaipanda; kileleni Yesu yuko tayari kuwapokea. Kuna malaika wanaowasaidia kupanda, na mashetani wanaojaribu kuwaangusha, hata kama wamepanda sana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Zecher, Jonathan L. (2013), "The Angelic Life in Desert and Ladder: John Climacus's Re-Formulation of Ascetic Spirituality", Journal of Early Christian Studies 21 (1): 111–136, ISSN 1086-3184, doi:10.1353/earl.2013.0006 
  2. Martyrologium Romanum
  3. Duffy, John (2010), "Reading John Climacus: Rhetorical Argumentation, Literary Convention and the Tradition of Monastic Formation (review)", Journal of Early Christian Studies 18 (1): 145–146, ISSN 1086-3184, doi:10.1353/earl.0.0303 
  4. Stroumsa, Guy (2008), "The Scriptural Movement of Late Antiquity and Christian Monasticism", Journal of Early Christian Studies (Johns Hopkins University Press) 16 (1): 61–77, ISSN 1086-3184, doi:10.1353/earl.2008.0011 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.