Yohane Almond

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yohane Almond (Allerton, karibu na Liverpool, Uingereza, 1577 hivi – London, 5 Desemba 1612) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki.

Baada ya kuhamia Ireland, aliingia seminari huko Roma, Italia, alipopata upadrisho mwaka 1598 kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali.

Alirudi Uingereza mwaka 1602 alipofanya uchungaji kwa siri hadi alipokamatwa na kuuawa kikatili sana.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[1].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.