WhatsApp

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
WhatsApp Messenger
Wandishi wa sasaWhatsApp Inc.
Tarehe ya kwanzaJanuari 2009; miaka 15 iliyopita (2009-01)
Lugha kompyutaErlang[1]
Mfumo wa uendeshajiAndroid, iOS, Windows Phone, BlackBerry OS, Symbian (kuna Windows, macOS, na tovuti programu pia, lakini tu na simu)
Aina ya programuMtandao wa kijamii
Leseni ya programuBure
Tovutiwhatsapp.com
WhatsApp
Tarehe ya kwanzaFebruari 24, 2009; miaka 15 iliyopita (2009-02-24)
Mwanzilishi
Pahali pa makao makuuMountain View, California, United States
Wafanyakazi50[2]
Mzazi ya shirikaFacebook
Tovutiwhatsapp.com
Mtu akituma ujumbe kwa kutumia WhatsApp.

WhatsApp ni mtandao wa kijamii unaotumika kutuma ujumbe wa maneno, sauti, picha au video unaomilikiwa na kampuni ya Facebook.[3]

WhatsApp inatumiwa hasa kwenye simu za mkononi ingawa inaweza pia kutumika kwenye kompyuta.[4]

Mwanzoni watumiaji walikuwa wanaweza kuwasiliana na watumiaji wengine mmoja mmoja au katika kundi lakini toka Septemba 2017 WhatsApp ilitangaza kuanzisha utaratibu wa makampuni kuwasiliana na wateja wao.[5]

Teknolojia hii ilianzishwa na kampuni ya WhatsApp Inc. ya Mountain View, California ambayo baadaye ilinunuliwa na Facebook mnamo Februari 2014 kwa gharama ya dola za Kimarekani bilioni 19.3.[6][7]

Hadi Februari 2018, WhatsApp ilikuwa na watumiaji zaidi ya bilioni moja na nusu. [8]

Teknolojia hii imeimarika katika nchi kadhaa kama vile Brazili, India, nchi kadhaa za Ulaya kama vile Uingereza na Ufaransa.[9]

Huduma ya kutumia WhatsApp kupiga simu ilianza kutumika Februari 2015. [10][11]. Tarehe 14 Novemba 2016 WhatsApp ilianzisha huduma ya kupiga simu kwa video kwa simu zinazotumia android, simu za iPhone na Windows.[12]

Tarehe 18 Januari 2016, mwanzilishi wa WhatsApp Jan Koum alitangaza kuwa kampuni hii haitatoza dola 1 ya Marekani kwa matumizi ya WhatsApp mwaka mmoja ili kuondoa tatizo lililokuwa linawasumbua watumiaji wasio na njia ya kulipa. Alitangaza pia kuwa kampuni hii haitaweka matangazo ya kampuni nyingine na badala yake itaimarisha huduma nyingine kama vile mawasiliano ya watumiaji na makampuni. Gharama ya WhatsApp huwa ni gharama watumiaji wanayolipa ili kutumia intaneti kwenye makampuni ya simu. Gharama hii hutofautiana kati ya nchi na nchi na pia kati ya kampuni za simu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

WhatsApp ilianzishwa na Brian Acton na Jan Koum mnamo mwaka 2009. Wote wawili walikuwa wafanyakazi wa zamani wa Yahoo! Kabla ya kuanzisha WhatsApp, waliona umuhimu wa kuwa na njia rahisi na ya haraka ya mawasiliano kwenye simu za mkononi.

WhatsApp ilitoka kama suluhisho la kutoza ada ya kila mwaka kwa watumiaji wake, badala ya kutegemea matangazo au mauzo ya data. Modeli hii ya biashara ilisaidia kudumisha faragha ya watumiaji kwa kiwango kikubwa. Huduma ilipata umaarufu haraka kutokana na urahisi wake wa matumizi, ujumuishaji wa nambari za simu kama kitambulisho, na uwezo wa kutoa mawasiliano ya haraka kwa njia ya ujumbe wa maandishi.

Mnamo mwaka 2014, WhatsApp ilinunuliwa na kampuni ya Facebook kwa dola bilioni 19. Hata baada ya ununuzi huo, WhatsApp ilijitahidi kudumisha sifa yake ya faragha na kutofautisha kati ya data ya WhatsApp na akaunti za Facebook. Hata hivyo, mabadiliko kadhaa yamefanywa kwa muda kuhusu sera za faragha, na mjadala kuhusu hili umeibuka mara kwa mara.

WhatsApp imeendelea kuwa mojawapo ya programu maarufu duniani kwa mawasiliano ya simu ya mkononi na inaendelea kuboreshwa na kupanuliwa na Facebook.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
 1. Ainsley O'Connell (Februari 21, 2014). "Inside Erlang, The Rare Programming Language Behind WhatsApp's Success". fastcompany.com. Iliwekwa mnamo Desemba 20, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 2. Metz, Cade (15 Septemba 2015). "Why WhatsApp Only Needs 50 Engineers for Its 900M Users". Wired. Condé Nast. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 3. Metz, Cade (5 Aprili 2016). "Forget Apple vs. the FBI: WhatsApp Just Switched on Encryption for a Billion People". Wired. Condé Nast. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. "WhatsApp FAQ - Using one WhatsApp account on multiple phones, or with multiple phone numbers". WhatsApp.com.
 5. "Building for People, and Now Businesses". WhatsApp.com.
 6. "Facebook's $18 Billion Deal Sets High Bar", February 20, 2014, pp. A1, A6. 
 7. Facebook to Acquire WhatsApp (Press release). February 19, 2014. http://newsroom.fb.com/News/805/Facebook-to-Acquire-WhatsApp.
 8. "WhatsApp hits 1.5 billion monthly users. $19B? Not so bad.", TechCrunch, 31 January 2018. Retrieved on 8 February 2018. 
 9. Metz, Cade (Aprili 5, 2016). "Forget Apple vs. the FBI: WhatsApp Just Switched on Encryption for a Billion People". Wired. Condé Nast. Iliwekwa mnamo Aprili 5, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 10. Chowdhry, Amit (26 Machi 2015). "WhatsApp For iOS Will Receive Voice Calling Feature In A Few Weeks". Forbes. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 11. Perez, Sarah (2 Februari 2015). "WhatsApp Voice-Calling Feature Spotted In The Wild". TechCrunch. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 12. "Whatsapp Video Calling" (blog). Iliwekwa mnamo Nov 18, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)