Jan Koum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faili:Tumblr inline n19k9vpY8G1qzzumw (cropped).jpg
Jan Koum(kushoto) na Brian Acton

Jan Koum (alizaliwa Februari 24, 1976) ni mtaalamu wa kompyuta Mmarekani mwenye asili ya Ukraine. Ni mmoja wa waanzilishi na alikuwa Mkurugenzi wa WhatsApp, ambayo ilinunuliwa na Facebook Inc. mnamo Februari 2014 kwa dola za Kimarekani bilioni 19.3.

Mwaka 2014, aliingia kwenye orodha ya Forbes ya watu tajiri 400 duniani akishika namba ya 62, akiwa na utajiri unaokadiriwa kuwa bilioni 7.5.[1]

Maisha ya mwanzo na kazi[hariri | hariri chanzo]

Koum alizaliwa Kiev, Ukraine. Ana asili ya Kiyahudi.[2] Alikulia Fastiv, nje ya Kiev, na baadaye akahamia Mountain View, California na mama na bibi yake mwaka 1992,[3] ambapo walipata msaada wa kijamii kwa kupewa nyumba ya vyumba viwili,[4] akiwa na miaka 16. Baba yake alikuwa amepanga kuwafuata Marekani lakini alibaki Ukraine,[5] na kufariki mwaka 1997.[4] Koum na mama yake waliendelea kuwa na mawasiliano naye hadi alipofariki.[6] Mwanzoni mama yake alifanya kazi ya uyaya wakati yeye alikuwa anafanya kazi ya usafi dukani. Mama yake alifariki mwaka 2000 baada ya kuugua ugonjwa wa kansa.

Alipokuwa na umri wa miaka 18 Koum alianza kuwa na shauku ya kujua masuala ya kuprogramu kompyuta. Alijiunga na chuo kikuu cha San Jose State University na wakati huo huo akifanya kazi Ernst & Young.[4]

Mwaka 1997, Koum alikutana na Brian Acton, mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, wakati akifanya kazi Ernst & Young.[4]

Yahoo![hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1997, Koum aliajiriwa na Yahoo! kama mhandisi. Aliacha shule muda mfupi baada ya hapo.[4] Kwa miaka tisa baadaye Koum and Acton walifanya kazi pamoja katika kampuni hiyo. Septemba 2007 waliacha kazi Yahoo! na kutembelea nchi kadhaa za Amerika ya Kusini na kucheza mchezo wa ultimate frisbee. Wote waliomba kazi katika kampuni ya Facebook lakini maombi yao yalikataliwa.[4]

WhatsApp na Facebook[hariri | hariri chanzo]

Januari 2009, Koum alinunua iPhone na hapo akatambua kuwa kampuni ya Apple ilikuwa ina mpango wa kutoa app mbalimbali. Alimtembelea rafiki yake Alex Fishman, huku wakinywa chai, walizungumza kwa masaa kadhaa juu ya wazo jipya alilokuwa nalo Koum.[4] Koum alichagua jina la WhatsApp kwasababu ilitamkika kama "what's up", na wiki moja baadaye wakati wa siku yake ya kuzaliwa, February 24, 2009, alisajili WhatsApp Inc. huko California.[4]

WhatsApp haikuwa maarufu hapo mwanzoni. Baadaye ilianza kupata watumiaji wengi na hapo akamshawishi rafiki yake Acton, ambaye alikuwa bado hajapata kazi, kujiunga na kampuni. Koum alimpa Acton hadhi ya mwanzilishi mwenza baada ya Acton kuipa kampuni dola za Kimarekani 250,000.[4]

Februari 9, 2014 Mark Zuckerberg alimwomba Koum kujiunga na bodi ya Facebook. Siku 10 baadaye Facebook ilitangaza kuinunua WhatsApp.[7][8][9][10][11]

Mnamo Aprili 30, 2018, Koum alitangaza kuondoka kampuni ya WhatsApp na pia bodi ya wakurugenzi wa Facebook kutokana na mgogoro na Facebook[12] It was originally thought that by leaving he was forfeiting his unvested stock, worth almost $1 billion.[13]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Forbes Announces Its 33rd Annual Forbes 400 Ranking Of The Richest Americans; 29 September 2014, Forbes.com, accessed 12 November 2014
 2. "WhatsApp Founder Jan Koum's Jewish Rags-to-Riches Tale", 20 February 2014. Retrieved on 1 March 2014. 
 3. Rowan, David. "WhatsApp: The inside story (Wired UK)". Wired.co.uk. Iliwekwa mnamo 2014-02-20. 
 4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 4.6 4.7 4.8 Parmy Olson. "Exclusive: The Rags-To-Riches Tale Of How Jan Koum Built WhatsApp Into Facebook's New $19 Billion Baby", Forbes, February 19, 2014. Retrieved on February 20, 2014. .
 5. WhatsApp: Jan Koum – The Story Of A Man Who Kept It Simple, Jewish Business News, Feb 20th, 2014
 6. Olson, Parmy. "Exclusive: The Rags-To-Riches Tale Of How Jan Koum Built WhatsApp Into Facebook's New $19 Billion Baby", Forbes. (en) 
 7. Olson, Parmy. "Exclusive: The Rags-To-Riches Tale Of How Jan Koum Built WhatsApp Into Facebook's New $19 Billion Baby", Forbes, 2009-02-24. Retrieved on 2014-02-20. 
 8. "Facebook acquires WhatsApp in massive deal worth $19 billion - ABC News (Australian Broadcasting Corporation)". Abc.net.au. Iliwekwa mnamo 2014-02-20. 
 9. "WhatsApp Founders Are Low Key — And Now Very Rich". Mashable.com. 2013-10-26. Iliwekwa mnamo 2014-02-20. 
 10. "WhatsApp's Founder Goes From Food Stamps to Billionaire". Bloomberg News. Iliwekwa mnamo February 20, 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
 11. Wood, Zoe. "Facebook turned down WhatsApp co-founder Brian Acton for job in 2009", The Guardian, February 20, 2014. Retrieved on 21 February 2014. 
 12. Dwoskin, Elizabeth. "WhatsApp founder plans to leave after broad clashes with parent Facebook", Washington Post, 2018-04-30. (en-US) 
 13. "Next change for Facebook: New board director, executives reshuffled", The Mercury News, 2018-05-08. (en-US) 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jan Koum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.