Utendi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Utendi ni aina ya ushairi na tanzu mojawapo ya fasihi simulizi. Kwa kawaida, utendi husimulia maisha na matendo ya mhusika shujaa au wa visasili. Ulaya, kuna tendi kama wimbo wa Troya, wimbo wa Odisei na wimbo wa kabila la Nibelungi; na India kuna wimbo wa Mahabharata. Hizo zote mara nyingi hudondolewa kama mifano ya utendi. Siku hizi hata riwaya au filamu, hasa kama ni ndefu sana pamoja na wahusika wengi au nyakati nyingi, huitwa utendi.