Audax Kahendaguza Vedasto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Audax Kahendaguza Vedasto (alizaliwa Nyakabanga, wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, 21 Agosti 1971) ni mwanasheria msomi aliyejikita katika tasnia ya uandishi wa vitabu vya sheria na diwani za mashairi. Kama ilivyo kwa washairi wengine, Audax hujulikana kwa lakabu ya ushairi kama "Mwana wa Kahenda".

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mwana wa Kahenda alianza masomo yake katika shule ya msingi Nyakabanga mwaka 1980 na kuhitimu mwaka 1986 ambapo mwaka 1987 alijiunga na masomo ya secondary katika shule ya upili ya Kahororo,na mwaka 1991 aliendelea mbele zaidi na kujiunga na elimu ya juu secondary katika shule ya Milambo akichukua masomo ya lugha,Kiswahili kingereza na kifaransa na kumaliza mwaka 1993 na kuvunja rekodi ya kuongoza kitaifa katika matokeo hayo kitaifa.

Mwaka 1993 alijiunga na mafunzo ya kijeshi katika jeshi la kujenga taifa katika kambi ya JKT Oljoro iliyopo mkoani Arusha

Ushairi[hariri | hariri chanzo]

Safari yake ya ushairi ilianza mwaka 1983 akiwa mwanafunzi wa darasa la nne kilichomvutia zaidi kuingia katika tasnia ya ushairi ni kupendelea kusoma vitabu huku shairi lililomvutia zaidi na kujikuta anazama katika ulimwengu wa ushairi ni shairi la Sizitaki Mbichi Hizi, moja kati ya mashairi maarufu Tanzania.

Shairi lake la kwanza kutunga lilikuwa linaitwa Nazitaka Mbichi Hizi ikiwa ni majibu ya shairi la Sizitaki mbichi hizi lakini kwa bahati mbaya shairi hilo lilipotea katika ajali ya meli ya MV Bukoba.

Uandishi wa vitabu[hariri | hariri chanzo]

Mbali na sheria, Audax Kahendaguza Vedasto ameandika diwani mbili hadi sasa, ya kwanza mwaka 2009 na inajulikana kama Mwanangu Nakuusia ukiwa ni utenzi, na diwani ya pili ilitoka mwaka 2010 kinakwenda kwa jina la Chopikwa Kikapikika [1] [2].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Audax Kahendaguza Vedasto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.