Diwani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Diwani nchini Tanzania ni mwakilishi wa wananchi wa kata yake, pia ni mwakilishi wa wananchi katika vikao vya baraza la madiwani la halmashauri anayoitumikia (halmashauri ya wilaya/manispaa/jiji/mji) kama ilivyoridhiwa katika sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa ya mwaka 1977 sura No.292-14(1).

Diwani pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (ward development committee, WDC) kama ilivyoandikwa katika sheria ya serikali za mitaa No.7(31) ya mwaka 1982, iliyofanyiwa marekebisho na sheria No.6 ya mwaka 1999.

Diwani pia ni mtunzi, mpitishaji, mwidhinishaji na msimamizi wa sheria ndogondogo zinazotungwa kwenye kata yake kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo kama ilivyoridhiwa katika sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1977 sura No.287-153(1) [mamlaka ya mji] na katika sura No.288-89 na 122(1) (d) [mamlaka ya wilaya].

Scale of justice 2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Diwani kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.