Chopikwa Kikapikika
Chopikwa Kikapikika ni diwani ya mashairi iliyotungwa na Audax Kahendaguza Vedasto, mshairi, mwanasheria na mwandishi wa vitabu vya sheria na tungo za mashairi [1]
Diwani ya Chopikwa Kikapikika [2] ilianza kuandikwa mwaka 1983 ikachapishwa miaka ishirini na saba baadaye katika mwaka wa 2010 ikiwa imejumuisha mashairi ya aina mbalimbali yaliyo katika lugha ya Kiswahili, huku shairi moja lenye beti moja likiwa limewekwa katika lugha ya Kihaya.
Kitabu hicho kimejumuisha mashairi ya kijamii yaliyolenga siasa, mapenzi, jeshi huku kikizungumzia sana kuhusu Jeshi la Kujenga Taifa na ngonjera moja iliandikwa ikizungumzia kuhusu JKT na michezo.
Mbali na kuzungumzia mambo hayo ya kijamii, diwani hiyo imegusia historia ya matukio yaliyokuwa yanatokea katika wilaya ya Nyakabanga, mkoa wa Kagera.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Audax – AUDA & COMPANY ADVOCATES" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-24. Iliwekwa mnamo 2020-02-24.
- ↑ Vedasto, Audax Kahendaguza. (2010). Chopikwa kikapikika. Dar es Salaam, Tanzania: Idea International Publishers. ISBN 978-9987-9220-5-5. OCLC 719673635.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chopikwa Kikapikika kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |