Utenzi wa Hati na Adili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utenzi wa Hati na Adili ni mfululizo wa tenzi mbili alizoziandika Shaaban Robert kwa watoto wake wawili Mwanjaa na Suleyman baada ya kifo cha mama yao Amina Bint Kihere kilichotokea mwaka 1942 [1]

Mwanjaa alitungiwa utenzi unaoitwa Hati na Suleyman alitungiwa utenzi unaoitwa Adili [2]

Katika tenzi hizo mbili Shaaban Robert alisisitiza watoto wake wasome sana elimu. Kama inavyojulikana, Shaaban Robert alikuwa akipenda sana watoto wake wasome na hata mwaka 1959 alishindwa kuhudhuria mkutano wa washairi ulioitishwa na Kaluta Amri Abeid na ulioshirikisha washairi maarufu wa Tanganyika.

Katika kuonyesha umuhimu wa elimu kwa watoto wake, mwaka 1945 Shaaban Robert aliamua kuomba uhamisho wa kazi kutoka Mpwapwa hadi Tanga ili kumtafutia mwanae wa kike sehemu salama ya kusoma, baada ya binti yake huyo kuwa miongoni mwa wasichana watano walofaulu mtihani wa darasa la nne na kufanikiwa kuingia darasa la tano.

Katika moja ya kusisitiza elimu kwa mwanawe, katika utenzi wa Hati, Shaaban Robert alitoa beti hizi:

30. Jifunze pata elimu,

Uwe mtu taalamu,

Halali na haramu,

Uweze kupambanua.

31. Elimu kitu kizuri,

Kuwa nayo ni fahari,

Sababu humshauri,

Mtu la kutumia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Robert, Shaaban, 1909-1962. (1991). Maisha yangu : na, Baada ya miaka hamsini (toleo la New ed). Dar es Salaam: Mkuki na Nyota. ISBN 9976-973-16-0. OCLC 34708545. 
  2. Robert, Shaaban, 1909-1962. (2003). Barua za Shaaban Robert, 1931-1958. Mulokozi, M. M. (Mugyabuso M.), Ulenge, Yusuf, 1917-, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam, Tanzania: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. ISBN 9976-911-62-9. OCLC 54023065. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utenzi wa Hati na Adili kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.