Kaluta Amri Abeid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Shekhe Kaluta Amri Abeid (mkoa wa Kigoma, 1924 [1] - 1 Januari 1964) alikuwa meya wa kwanza Mwafrika [2] na mwanasiasa pamoja na mhubiri wa dini.

Kwa jina la utani la kishairi alikuwa akijulikana kama Adili, lakini katika kipindi cha utoto wake baba yake alipenda kumuita kwa jina la Simba wa Lumona [3][4], kama ilivyo kwa washairi wengi kutumia majina ya utani au lakabu.

Baba yake alijulikana kama Abeid Kaluta na mama yake alijulikana kama Joha Kakolwa,

Uwanja maarufu wa mpira katika mkoa wa Arusha hujulikana kama uwanja wa kumbukumbu wa Shekhe Amri Abeid, ni uwanja ulopewa jina la mwanasiasa na mshairi huyu mkubwa nchini Tanzania [5].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tarehe rasmi na mwezi wa kuzaliwa vimekuwa havijulikani kutokana na kutokutunzwa vyema kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
  2. Mwalimu J.K.Nyerere na Kaluta Amri Abeid (en). Mwananchi. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-01-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-27.
  3. Simba wa Lumona ni jina linalotokana na mtemi maarufu aliyekuwepo katika nchi ya Congo na aliyetokana na vizazi vya Pole
  4. ISBN 978-9987-9650-2-1
  5. Hivi viwanja vione tu, ni majina ya watu na mitaa (en). Mwanaspoti. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-01-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-27.