Simoni wa Rojas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Simoni akilisha fukara.

Simoni wa Rojas (Valladolid, Hispania, 28 Oktoba 1552 - Madrid, 29 Septemba 1624) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.

Ingawa kwa miaka mingi alitakiwa kuongozana na malkia na kuishi ikulu, alizidi kuishi kwa unyenyekevu na ufukara, akimheshimu Bikira Maria kwa namna ya pekee[1].

Alitangazwa na Papa Klementi XIII kuwa mwenyeheri tarehe 19 Machi 1766, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 3 Julai 1988.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Septemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91616
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Matthew Bunson, Margaret Bunson, Our Sunday Visitor's Encyclopedia of Saints, Our Sunday Visitor Publishing, p 757.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.