Paulo Miki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtakatifu Paulo Miki

Mtakatifu Paulo Miki (takriban 1565 – 5 Februari 1597) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Japani.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Paulo Miki alizaliwa nchini Japani kati ya 1564 na 1566.

Alijiunga na Shirika la Yesu (Wajesuiti), akahubiri Injili kwa ufanisi.

Lakini yalipoanza madhulumu kwa Wakatoliki, yeye na wenzake 25 walikamatwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597.

Hadi sasa Wafiadini wa Japani waliotangazwa watakatifu ni 42, mbali na wenye heri 393.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1282
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paulo Miki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.