Petro Sukejiro
Mandhari
Petro Sukejiro alikuwa katekista wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko aliyefia dini nchini Japani (1597).
Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kati yao Paulo Miki, Yohane wa Goto na Yakobo Kisai walikuwa Wajesuiti; Petro Baptista, Martino wa Kupaa na Fransisko Blanco, walikuwa mapadri wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku; Filipo wa Yesu, Gonzalo Garcia na Fransisko wa Mt. Mikaeli walikuwa mabradha wa shirika hilohilo; Leo Karasuma, Kosma Takeya, Paulo Ibaraki, Tomaso Danki, Paulo Suzuki walikuwa makatekista Wajapani; Ludoviko Ibaraki, Antonio, Mikaeli Kozaki na mwanae Tomaso, Bonaventura, Gabrieli, Yohane Kinuya, Matia, Fransisko wa Meako, Yohakimu Sakakibara na Fransisko Adaukto walikuwa Wakristo wapya.
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |