Petro Baptista
Mandhari

Petro Baptista (kwa Kihispania San Pedro Bautista), alikuwa balozi wa Hispania nchini Japani, mkuu wa Ndugu Wadogo Pekupeku wamisionari huko, padri aliyehudumia wakoma, na hatimaye akawa kiongozi wa wafiadini 26[2] waliouawa msalabani tarehe 5 Februari 1597 [3].
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 14 Septemba 1627, halafu Papa Pius IX akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Juni 1862.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/93366
- ↑ Kati yao Paulo Miki, Yohane wa Goto na Yakobo Kisai walikuwa Wajesuiti; Martino wa Kupaa na Fransisko Blanco, walikuwa mapadri wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku; Filipo wa Yesu, Gonzalo Garcia na Fransisko wa Mt. Mikaeli walikuwa mabradha wa shirika hilohilo; Leo Karasuma, Petro Sukejiro, Kosma Takeya, Paulo Ibaraki, Tomaso Danki, Paulo Suzuki walikuwa makatekista Wajapani; Ludoviko Ibaraki, Antonio, Mikaeli Kozaki na mwanae Tomaso, Bonaventura, Gabrieli, Yohane Kinuya, Matia, Fransisko wa Meako, Yohakimu Sakakibara na Fransisko Adaukto walikuwa Wakristo wapya.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/22072
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 47
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 426-428
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |