Nenda kwa yaliyomo

Yohane wa Goto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yohane wa Goto (takriban 15785 Februari 1597) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Japani.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari[1].

Alizaliwa nchini Japani akajiunga na Shirika la Yesu (Wajesuiti) muda mfupi kabla hajauawa.

Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[2]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.

Hadi sasa Wafiadini wa Japani waliotangazwa watakatifu ni 42, mbali na wenye heri 393.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1282
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.