Nenda kwa yaliyomo

Nyigu-msumeno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyigu-msumeno
Arge humeralis
Arge humeralis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Symphyta (Hymenoptera wasio na kiuno chembamba sana)
Gerstäcker, 1867
Ngazi za chini

Familia za juu 6; 4 na familia 5 katika Afrika:

Nyigu-msumeno (kutoka kwa Kiing. sawflies) ni wadudu wa nusuoda Symphyta katika oda Hymenoptera walio na mrija wa kutagia mayai ufananano na msumeno. Hawana kiuno chembamba sana kama nyigu wa kawaida. Spishi za familia Siricidae huitwa nyigu-ubao pia na zile za Orussidae ni vidusia wa lava wa mbawakawa na nyigu ambao huishi ndani ya ubao wa miti. Nusuoda hii ina takriban spishi 8000 duniani kote na zaidi ya 90 katika Afrika ya Mashariki.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nyigu-msumeno wengi sana wana urefu wa mm 2.5-20, ingawa wengine wanaweza kufikia mm 55. Wanafanana na nyigu wa kweli kwa kiasi fulani, lakini hawana kiuno chembamba cha hao[1]. Mrija wao wa kutagia ni kama msumeno ili kukata ndani ya tishu za mimea. Baadhi ya nyigu-msumeno huiga nyigu au nyuki ili kupunguza uwindaji na mrija wao wa kutagia unaonekana kama mwiba.

Lava wa nyigu-msumeno ndani ya bua la mwaridi)
Kundi la lava.

Majike hutumia mrija wa kutagia kama msumeno ili kukata ndani ya bua la mmea au shina la mti na kutaga mayai. Lava wanaonekana kama viwavi lakini wana miguu ya bandia zaidi, ambayo pia haina ndoano. Wengi sana hula majani huku wengine wakila ndani za mabua ya mimea. Lava wa Siricidae hula ubao na wale wa Orussidae hula mabuu ya mbawakawa na nyigu wanaokula ubao. Lava wanaoishi huru hula mara nyingi katika makundi mazito ili kuzuia uwindaji.

Wapevu wa nyigu-msumeno huishi siku 7-9 tu, lakini lava wanaweza kudumu kutoka miezi hadi miaka kadhaa kulingana na spishi. Majike wengi wanaweza kutaga mayai yanayoendelea bila madume, yaani wao ni pathenojenetiki. Hata hivyo, spishi nyingine nyingi bado zina madume. Wapevu hula mbelewele, mbochi, mana ya wadudu, utomvu au hemolimfu ya wadudu wengine.

Baadhi ya spishi, kama vile nyigu-msumeno wa misonobari, zinaweza kusababisha hasara kubwa wakati idadi ya wadudu inakua kubwa sana, kwa kutoa majani ya miti na kusababisha kudumaa kwa ukuaji na hata kifo[2]. Hata hivyo, kwa ujumla, nyigu-msumeno wana umuhimu mdogo wa kiuchumi.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

 • Aethiocampa aethiopica
 • Afrotremex comatus
 • Arge bipartita
 • Arge deckerti
 • Arge elisurbis
 • Arge imbecilla
 • Arge marshalli
 • Arge micheli
 • Arge octava
 • Arge orientalis
 • Arge prima
 • Arge rothschildi
 • Arge stuhlmanni
 • Arge taitaensis
 • Arge ugandana
 • Arge uncina
 • Athalia armata
 • Athalia atripennis
 • Athalia cerberus
 • Athalia clavata
 • Athalia concors
 • Athalia deckerti
 • Athalia excisa
 • Athalia flavobasalis
 • Athalia furcipennis
 • Athalia fuscata
 • Athalia marginipennis
 • Athalia melanopoda
 • Athalia nigripes
 • Athalia pluto
 • Athalia pulla
 • Athalia pullicoma
 • Athalia schweinfurthi
 • Athalia segregis
 • Athalia sjoestedti
 • Athalia taitaensis
 • Athalia truncata
 • Athalia umbrosa
 • Athalia ustipennnis
 • Athalia vollenhoveni
 • Athalia zanzibarica
 • Chalinus imperialis
 • Chalinus plumicornis
 • Distega abdominalis
 • Distega clypealis
 • Distega humeralis
 • Distega montium
 • Distega pallidiventris
 • Dulophanes abdominalis
 • Dulophanes antennatus
 • Dulophanes atratus
 • Dulophanes flavipes
 • Dulophanes gowdeyi
 • Dulophanes pedicellatus
 • Kivua abdominalis
 • Kivua cara
 • Kivua cribrifrons
 • Kivua incassata
 • Kivua pallipes
 • Kivua tenuis
 • Leptorussus africanus
 • Muncheana mandibularis
 • Neacidiophora athaloides
 • Neacidiophora bellicornis
 • Neacidiophora bequaerti
 • Neacidiophora brevifalcata
 • Neacidiophora obscurus
 • Neacidiophora silacea
 • Neacidiophora ugandae
 • Pampsilota afra
 • Pampsilota africana
 • Pampsilota tsavoensis
 • Pampsilota zebra
 • Pseudoneacidiophora bicolor
 • Pseudoneacidiophora pleuritica
 • Sjoestedtia meruensis
 • Trisodontophyes angustata
 • Trisodontophyes antennata
 • Trisodontophyes diversa
 • Trisodontophyes malaisei
 • Trisodontophyes montana
 • Trisodontophyes robusta
 • Trisodontophyes ugandae
 • Xenapates aequatorialis
 • Xenapates bequaerti
 • Xenapates braunsi
 • Xenapates flavus
 • Xenapates gaullei
 • Xenapates insignitus
 • Xenapates nigrifrons
 • Xenapates nigritus
 • Xenapates offrenatus
 • Xenapates variator
 • Xenapates ventralis
 • Xenapates virgatus

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Goulet, H.; Huber, J.T. (1993). Hymenoptera of the World: An Identification guide to families (PDF). Ottawa, Ontario: Agriculture Canada. ISBN 978-0-660-14933-2. Archived from the original (PDF) on 5 March 2016 https://web.archive.org/web/20160305012733/http://www.esc-sec.ca/aafcmonographs/hymenoptera_of_the_world.pdf.
 2. Krokene, Paal (6 December 2014). "The common pine sawfly – a troublesome relative". Science Nordic. Retrieved 28 November 2016.